Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Breaking News: Chelsea Yamtimua Frank Lampard

KLABU ya soka ya Uingereza, Chelsea,  imemfuta kazi kocha wake mkuu, Frank Lampard, kutokana na mwendelezo mbaya wa matokeo ya mechi za mashindano mbalimbali za katika klabu hiyo.

 

Kwa mujibu wa mmiliki wa klabu hiyo, imefafanua kuwa maamuzi hayo yamefikiwa kutoka pande zote ikiwemo bodi na mmiliki wa timu hiyo, Roman Abramovic ambapo amesema, imekuwa lazima kufanya uamuzi huo mgumu huusani kutokana na matokeo mabaya ya hivi karibuni yaliyoifanya klabu hiyo kushuka hadi nafasi za katikati.

 

“Huu ulikuwa uamuzi mgumu kwa Klabu kwani nina uhusiano mzuri na Frank na ninamheshimu,” alisema Abramovich akiongeza kwamba pamoja na umahiri wake mazingira ya sasa yamelazimu kubadili kocha.

 

Klabu hiyo haitatoa taarifa yoyote hadi hapo atakapopatikana kocha mwingine. Taarifa zinazoendelea kuvuma katika mitandao mbalimbali nchini Uingereza zinasema kuwa aliyekuwa kocha wa PSG na Borrusia Dortmund, Thomas Tuchel anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Lampard.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments