Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Breaking News: JPM Aagiza Daktari Aliyeacha Kazi Asakwe "Wanakuwa Wabinafsi Sana"

 


RAIS  John Magufuli amemwagiza Waziri wa Afya, Dkt Dorothy Gwajima, kuhakikisha anawafuatilia madaktari walioacha kazi katika hospitali ya rufaa mkoa wa Tabora kwa sababu ya maslahi na kuhamia hospitali binafsi na ikiwezekana wafungiwe pamoja na hospitali walizokimbilia.


Ametoa amri hiyo kufuatia kuondoka kwa daktari mmoja katika hospitali hiyo ya mkoa na kwenda katika hospitali binafasi.
 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 30, 2021, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika hospitali hiyo na kwamba haiwezekani serikali ipoteze pesa kwa ajili ya kusomesha madakatari na wao badala ya kuwatumikia wananchi wanaanza kuwa wabinafsi kwa kutaka maslahi makubwa.


“Mfuatilie huyo daktari aliyekimbia hapa, uifuatilie na hiyo hospitali ikiwezekana tunamfungia huyo daktari na tunaifungia na hiyo hospitali aliyoenda kutibia ili watu waanze kujifunza kwamba wizara ya afya siyo ya kuchezea tu, unamsomesha mtu kwa fedha za Watanzania halafu anasema maslahi madogo”, amesema  Magufuli.


Aidha aliongeza: “Madaktari wote wanapata mkopo kwa asilimia 100, unasoma pale kwa miaka mitano ukishatoka pale unasema maslahi madogo, si ungekimbia wakati unasoma?  Hela yetu umekula halafu unasema maslahi madogo, nia ya serikali ni kuboresha maslahi lakini unaanza na kimoja, unaboreshaje maslahi wakati huna majengo wala vifaa vya kutosha?”

VIDEO:


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments