google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Chatu Wawa Tishio Bunju B, Wananchi Waingia Porini Kuwasaka | UDAKU SPECIAL

Chatu Wawa Tishio Bunju B, Wananchi Waingia Porini Kuwasaka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wananchi wa eneo la Kitunda Mtaa wa Bunju B, Kata ya Mabwepande, Kinondoni, Jijini Dar es Salaam, wameiomba serikali kuwasaidia baada ya kuishi kwa hofu kutokana na tishio la chatu.

Wananchi hao walitoa kilio hicho leo katika kikao kilichoitishwa na Diwani wa Kata ya Mabwepande Mhajilina Kassim maarufu kama Obama. Mkutano huo ulianza kwa wananchi hao kufanya usafi katika eneo itakapojengwa Shule ya Msingi Bunju B ambapo walifyeka eneo hilo ili kuanza ujenzi.

Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako Kirahisi




Pia wakiongozwa na diwani huyo walifanya msako wa chatu kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi. Walisema licha ya chatu pia kwenye eneo hilo wameonekana wanyama wakali kama vile chui na mamba.

Akizungumza na wananchi hao, Diwani Kassim alisema anamini serikali ni sikivu itawasaidia kukabiliana na tishio la chatu hao wanaodaiwa kuzagaa mtaani.


Obama aliszema chanzo cha kuzaliana kwa chatuni na wanyama wakali katika eneo hilo ni kuwepo kwa pori ambalo lina mgogoro kwa miaka zaidi ya saba.



Alisema pori hili liko karibu na eneo ambalo shule ya msingi itajengwa, hivyo kuiomba serikali kuingilia kati ili kesi ya mgogoro wa eneo hilo iliyopo Mahakama Kuu ya Ardhi kumalizika.

“Hatuna mamlaka ya kuingilia kati kesi ila tutaiandikia maombi mahakama ituruhusu kufyeka eneo hili ili kuepusha chatu kuzaliana,”alieleza Obama.


Alisema tayari Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetoa Sh. Milioni 156 kujenga madarasa tisa katika eneo hilo.
“Hatuna shule hapa Kitunda, shule ipo upande wa pili wa Barabara ya Bagamoyo, Mtaa wa Kiyonzile, hivyo ujenzi wa shule hii mpya ni muhimu ili kuepusha watoto kugongwa na magari au tishio hili la chatu na wanyama wakali.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bunju B, Athuman Njama , alithibitisha wananchi wake kuishi katika tishio la chatu hao aliodai wanalanda mara kwa mara mtaani.
“Wananchi wanaishi kwa hofu hapa.Wengi wanajifungia mapema ndani,”alisema Njama. Aliongeza: “Tunaomba serikali ije itusaidie kuwinda wanyama hawa.”


Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako Kirahisi




Mzee Asheli Ishiriyo, mkazi wa eneo hilo alisema hivi karibuni chatu mkubwa alikutwa akimmeza mbwa katika banda la jirani yake.

“Alikuwa ni mkubwa kama nguzo ya umeme. Alipo tuona alimtema mbwa na kutuvimbia ili kukabiliana na sisi. Tukakimbia,”alieleza mzee huyo. Ally Said, alisema mwezi mmoja uliopita walifanikiwa kumuua chatu mmoja na kumzika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad