Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Chuchu Awaponda Mastaa Wanaozindua Miradi FekiMSANII wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans amewaponda mastaa wenzake wanaozindua miradi mbalimbali ikiwemo maduka na saluni wakijifanya miradi yao kumbe si kweli isipokuwa wanataka kuipa ustaa miraji hiyo.


Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Chuchu alisema utasikia mara staa fulani kazindua duka lake la viatu maeneo fulani mara mwingine kazindua saluni yake eneo fulani lakini baada ya muda unakuja kugundua kumbe hakuna lolote.


“Utasikia fulani kazindua duka la viatu maeneo fulani mara mwingine kafungua saluni ya kisasa maeneo fulani tena wakitaja mpaka thamani ya hiyo miradi lakini baada ya muda unakuja kugundua kumbe hiyo ilikuwa ni kuipa kiki miradi hiyo.


“Mimi nimeamua kuiboresha saluni yangu hapa Sinza White Inn na nnaposema saluni yangu namaanisha yangu na sio kujipazia kwa ajili ya kuipa ustaa mimi siyo kama hao,” alisema Chuchu.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments