Chuchu, Ray Ndo Basi Tena!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


MSANII wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans amesema kuzaa na msanii mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray’ isiwe tabu na kuanza kumjulisha kila kinachoendelea katika maisha yake na kumtaka mengine ajionee sapraizi.

 

Wasanii hao waliachana mazima ambapo kwa sasa kila mtu anaishi kivyake lakini kama wasemavyo Waswahili, waliozaa hawaachani lakini Chuchu amepingana na usemi huo kwa kusema hiyo ndiyo imetoka mazima.

 

Amesema hawezi kufikiria kuanza kumjulisha kwa kila anachotaka kukifanya kwa ajili ya maendeleo yake eti kisa amezaa naye.

Hivi karibuni Chuchu aliifanyia maboresho saluni yake iliyopo Sinza White Inn na kuongeza sehemu ya studio ya muvi, masaji na sehemu maalum ya kuwarembea mastaa.


Licha ya kufungua mradi mkubwa kama huo paparazi wetu alimuuliza kama huenda amemshirikisha kwa lolote mzazi mwenzake huyo lakini Chuchu amesema hakuwa na sababu ya kufanya hivyo na kumtaka iwe sapraizi kwake.“


Sina sababu ya kumshirikisha kwenye mambo yangu, kuzaa isiwe tabu mimi na yeye tumeshaachana kila mtu anaishi kivyake hivyo kama dili zangu acha ajionee sapraizi kwenye vyombo vya habari lakini siyo mimi kuanza kumpa taarifa,” alimaliza kusema Chuchu.


Stori:Richard Bukos

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad