1/15/2021

Dar, Bagamoyo Vinara Matokeo Kidato cha Nne 2020

HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani imeshika nafasi ya kwanza kati ya Halmashauri 10 zilizofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2020 huku ikifanikiwa kuingiza shule mbili kati ya shule 10 bora kitaifa.

 

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo (Januari 15, 2021) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk Charles Msonde, amezitaja halmashauri nyingine zilizofanya vizuri kuwa ni Bukoba Mjini ya mkoani Kagera iliyoshika nafasi ya pili.

 

​Halmashauri nyingine ni Meru (Arusha), Njombe (Njombe), Bariadi (Simiyu), Kibondo (Kigoma), Moshi Manispaa (Kilimanjaro), Kibaha (Pwani), Moshi (Kilimanjaro) na nafasi ya 10 inashikiliwa na Mtwara Mjini ya mkoani Mtwara.

 

Katika matokeo hayo ya kidato cha nne mikoa ya Pwani na Kilimanjaro imefanikiwa kuingiza halmshauri mbili kila mmoja.

Wakati Bagamoyo ikishika nafasi ya kwanza kitaifa, pia imefanikiwa kuingiza shule mbili za Ahmes na Marian Boys katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo hayo.

 

Katika ngazi ya mkoa, Arusha ndiyo imeongoza kitaifa kwa ufaulu ikifuatiwa na Kilimanjaro ambao umeangushwa kutoka nafasi ya kwanza ulioshika mwaka juzi. Mkoa mwingine ambao umefanya vizuri katika matokeo hayo ni Iringa ambao ulikuwa na shule 165 zilizoshiriki mtihani huo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger