1/24/2021

Davina Anika Maumivu Ya Kukosa Ubunge

MIONGONI mwa waigizaji wa kitambo ambao bado wanafanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo Movies ni Halima Yahya. Mashabiki wake lukuki tangu enzi za Kaole Sanaa Group, wanamjua kwa jina la Davina.

 

Amekuwa akivaa uhusika vilivyo na kuzitendea haki scenes (vipengele) vyote anavyopewa kwenye uigizaji.

 

Davina ni mwanamama mwenye mvuto na mwonekano wake wa kipekee. Amewahi kutamba na sinema kama Stupid Father, Mjomba, Taariku Salaa na nyingine kibao.

 

Gazeti la IJUMAA linamsogeza Davina karibu karibu yako baada ya kufanya nae mahojiano maalum (exclusive interview) ambapo ameanika mengi ikiwemo ishu ya kukosa Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM);IJUMAA: Mambo vipi Davina?

 

DAVINA: Salama kabisa, Mwenyezi Mungu anasaidia.IJUMAA: Hongera kwa kuthubutu kuwania Ubunge wa Viti Maalum…

DAVINA: Ahsante sana.

 

IJUMAA: Je, una lipi la kuzungumza juu ya kukosa nafasi hiyo muhimu ya kuwa mbunge?

DAVINA: Kwanza ninamshukuru sana Mungu mpaka hapa nilipofikia kwa sababu ilikuwa kazi sana. Ujue mimi siyo mzoefu sana kwenye masuala ya siasa hivyo nilipitia kwenye maumivu mengi, ila ninaamini kwamba huu ni mwanzo mzuri kwangu.

IJUMAA: Unadhani mbunge aliyeshika nafasi yako ana vigezo vya kuwa kwenye nafasi hiyo?

 

DAVINA: Kwa hapo mimi sina cha kusema maana wanaojua kwamba mtu f’lani anaweza ni wananchi ndiyo maana wamemchagua huyo.

 

⚫️ Kwa UPDATES za Mastaa, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

IJUMAA: Vipi miaka ijayo utagombea tena au ndiyo basi?

 

DAVINA: Huu siyo mwisho, lazima nitaweza kugombea tena miaka ijayo maana napenda sana kuwa kwenye mambo ya siasa. Kuna mambo mengi niliyoweka ahadi kuwafanyia wananchi kama nikipata uogozi. IJUMAA: Mambo gani tena hayo ambayo unatamani kuyafanya?

 

DAVINA: Ya kuweza kusaidia jamii inayonizunguka na vitu vingine vingi.

IJUMAA: Unazungumziaje uongozi wa Rais Dk Mgafuli?

DAVINA: Anastahili kuwa kiongozi kwa sababu ana vigezo vyote. Pia ni mtu ambaye anakubalika sana, anatenda haki bila kujali wadhifa wa mtu.

 

IJUMAA: Tukirudi kwenye sanaa yako ya uigizaji, hali iko vipi kwa sasa?DAVINA: Hali iko poa kabisa, mambo yanaenda kama yalivyopangwa.

IJUMAA: Wasanii wengi sasa hivi wamejikita kwenye tamthiliya zao, kuna siri gani ambayo imejificha nyuma ya pazia?

 

DAVINA: Tamthiliya ni kitu ambacho kiko vizuri sana kwa sasa hivi, huwezi kulinganisha na filamu.

 

IJUMAA: Kuna taarifa njema kwamba tamthiliya zinalipa kuliko filamu, je, hapo kuna ukweli wowote?

DAVINA: Ndiyo, tamthiliya zinalipa sana sasa hivi ndiyo maana hata sisi waigizaji tumeamu kukomaa nazo.

 

⚫️ Kwa UPDATES za Mastaa, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

IJUMAA: Kwenye sanaa ya uigizaji wa sasa hivi, unaonaje upepo ukilinganisha na kipindi cha nyuma?

DAVINA: Kwa sasa hivi upepo siyo mzuri kabisa, soko siyo zuri kama zamani.

IJUMAA: Kwa nini soko siyo zuri kama zamani na unadhani waigizaji huwa mnafeli wapi?

DAVINA: Siyo kwamba tunafeli. Sababu ni kwamba tunauza hapahapa ndani ya nchi ya yetu, bado hatujapata tobo la kwenda nje ya mipaka yetu zaidi.

 

IJUMAA: Kwani hamjawahi kujaribu na masoko ya nje muone hali iko vipi?

DAVINA: Bado hatujaweza kujaribu kwa nje ya nchi.

IJUMAA: Kwa nini msijaribu na masoko ya nje muangalie itakuwaje?

DAVINA: Hapo ni kazi ya wasimamizi.

IJUMAA: Sanaa kwa upande wako imekunufaisha kiasi gani?

DAVINA: Nimenufaika na mambo mengi sana, ila kikubwa ni kwamba nimeweza kujulikana na watu wengi ndani na hata nje ya nchi.

IJUMAA: Kwa sasa mnafanya kazi na wasanii wa Bongo Fleva, labda nini siri ya kufanya hivyo?

DAVINA: Hakuna siri yoyote maana tangu mwanzo tulikuwa tunafanya nao, msani kama TID na wengine wanatokea kwenye Bongo Fleva, ila sema tu kwa sasa wamekuja kwa mwitikio mkubwa.

IJUMAA: Hivi ushawahi kufikiria kuachana na kuigiza?

 

DAVINA: Hapana, sijawahi kuwaza kabisa kuacha kuigiza maana mimi najua sanaa iliponitoa labda apende Mungu.

IJUMAA: Labda ikatokea mume wako akakutaka kuachana na kuigiza, utaweza kumpinga kwenye hilo?

 

DAVINA: Najua hawezi kunikataza kwa sababu anatambua ni kwa namna gani sanaa imeweza kunisaidia kwenye mambo f’lanif’lan.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger