Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Donald Trump Akubali Kuachia Madaraka Kwa Amani
Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza makabidhiano ya madaraka kwa njia iliyonyooka ifikapo Januari 20, baada ya mabaraza ya bunge kuthibitisha ushindi wa Rais mteule Joe Biden.
Trump amesema hakubaliani kabisa na matokeo ya uchaguzi hata hivyo kutakuwa na mapokezano ya madaraka kwa njia ya amani, ameyasema hayo huku akiendelea na madai yake kwamba uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.

Ameongeza kwamba japo hatua hiyo ni mwisho wa muhula wake wenye mafanikio makubwa katika historia ya Urais nchini Marekani, ni mwanzo tu wa mapambano wa kuifanya Marekani kuwa imara tena.

Taarifa hiyo ilitolewa kupitia ukurasa wa twitter wa mkurugenzi wake wa mitandao ya kijamii Dan Scavino kwa kuwa kurasa za Trump katika mitandao ya Twitter, Facebook na Instagram zimefungwa kwa muda kufuatia tukio la wafuasi wake kuvamia majengo ya bunge mjini Washington.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments