Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Dr. Dre Akubali Kumlipa MKE wake wa Zamani Bilioni 4 Kama Hela ya Matumizi ya Kila Siku


Licha ya kuwa anaendelea kupata nafuu mara baada ya jana kukimbizwa hospitali kutokana na matatizo kwenye ubongo, Dr. Dre amekubali kumlipa aliyekuwa mke wake, Nicole Young pesa za kutumia.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Blast jana (January 6), Dre alikubali kuwa anamlipa Nicole kiasi cha ($2 million) takribani Bilioni 4.6 za Kitanzania kama gharama za matumizi yake ya kila siku kwa miezi michache ijayo.


Shauri la talaka la wawili hao limesikilizwa jana na waliwakilishwa na wanasheria wao. Makubaliano hayo yanasema Nicole atapokea kiasi hicho cha fedha kuanzia Jumatatu ijayo (January 11) kumsaidia kwa ajili ya matumizi yake akiwa nyumbani kwake mjini Malibu. Japokuwa gharama za ulinzi zitakuwa juu yake hadi tena watakapo kutana mahakamani mwezi April.


Kwenye shauri hilo, Nicole ametoboa siri kwamba mtayarishaji huyo mkongwe ana kitita cha pesa taslimu ($250M) sawa na TSh. Bilioni 580 pia ana hisa kwenye Kampuni ya Apple.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments