Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Esma Ampinga Mama Mondi

MAMBO ni mengi muda ni mchache! Sekeseke aliloliamsha Mama Dangote, Sanura Kassim ‘Sandra’ limechukua sura mpya baada ya dada wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan kumpinga mama huyo, IJUMAA WIKIENDA lina habari mpya.

 

ISHU IMEIBUKA HIVI;

Kwenye sehemu ya mahojiano ambayo mama Diamond amekaririwa wakati akifafanua kuhusu suala la kwamba baba wa mwanaye Diamond siyo mzee Abdul Juma ndipo alipozua ubuyu mpya.“Jina la Nasibu Abdul nilimpa yeye (Abdul) kwa sababu yeye ndiye alinipeleka hospitali, alisema atamlea mtoto na mtoto hajamlea.“

 Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako Kirahisi


Hizo picha tunazopiga za ukubwani tulipiga tukiwa tunatoka Mtaa wa Somali (Kariakoo jijini Dar) kwa dada yangu, Mama Esma, dada yangu mimi…” Alikaririwa Mama Diamond.MTAFARUKU MPYA

Kitendo cha Mama Diamond au Mama Dangote kutamka kuwa, ‘tunatoka Mtaa wa Somali kwa dada yangu, mama Esma, dada yangu mimi…’ ndipo mitandaoni ‘kukachafuka’ upya na watu kuhoji kumbe Esma naye siyo mtoto wa Mama Diamond!“Heeh! Makubwa tena ina maana Yuda (Esma) kumbe naye siyo mtoto wa Mama Dangote, mji mzito huu,” maoni yaliyofanana na hayo ndiyo yalitawala kwenye mitandao ya kijamii hususan Istagram.

 

USHAHIDI WA PICHA SASA

Wengine walikwenda mbali zaidi kwa kuchukua picha za Esma na kusema ndiyo maana kweli hafanani na Diamond wala Mama Diamond.“Inawezekana jamani maana kweli Esma hafanani kabisa na Diamond wala mama yake. Inawezekana alimlea tu mtoto wa dada yake,” alichangia mdau mwingine.

 

MAMA DIAMOND ANA MTOTO MMOJA

Mjadala wa suala hilo ulizidi kuwa moto ambapo wadau wengine kwenye mitandao walisema kama Esma naye si mtoto wa Bi Sandra au Mama Dangote, basi mtoto pekee atakayekuwa wa kwake ni Diamond au Mondi.“Basi tena ina maana Mama Dangote ana mtoto mmoja tu mpaka sasa ambaye ni Diamond maana Esma ana mama na baba yake,” alishadadia mchangiaji mwingine.

HUYU HAPA

Baada ya mjadala huo kuwa mzito mtandaoni, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimsaka Esma ambaye alitoa maneno yaliyopingana na ya mama yake.

 Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako Kirahisi


ADAI WATU KUELEWA VIBAYA

Esma alisema kuwa kuhusu yeye kutokuwa mtoto wa Mama Dangote, watu wameelewa vibaya mama yake huyo kwa sababu yule ni mama yake mzazi, lakini alipokuwa mdogo alilelewa sana na mama yake mkubwa aitwaye Mama Mwajei mpaka watu wakawa wanamuita Mama Esma.“Yaani watu bwana, kwa hiyo wameshaona tena mimi siyo mtoto wa Mama Dangote, jamani, kama walisikia mama akisema Mama Esma ni sawa kwani ni mama yangu mkubwa ambaye amenilea mimi,” alisema Esma kwa jazba.

 

AKUMBUSHIA MENGINE

Esma aliongeza kuwa, hata huko nyuma, mama yake, DJ Rommy Jones (binamu wa Diamond) alimlea sana Diamond, mpaka wengine walijua ni mama yake hivyo watu watulie kwani yeye ni damu kabisa ya Mama Dangote.“Watu wakae kwa kutulia kabisa, mimi ni mtoto halisi kabisa wa Mama Dangote, hajasingiziwa mtu hata kidogo maana hata Mama Rommy Jones, wengi walikuwa wakijua ni mama yake Nasibu,” anasema Esma.

TUMEFIKAJE HAPA?

Kwa miaka mingi iliyopita, ilifahamika kuwa baba yake mzazi Diamond ni Abdul Juma almaarufu Baba D, lakini mwishoni mwa wiki iliyopita, Mama Diamond alichomoa betri kwa kumtaja baba halisi wa Diamond kuwa ni marehemu Sulum Idd Nyange.Hapo ndipo tifu liliposhika moto ambapo mijadala ikawa mingi mitandaoni, mzee Abdul Juma akaibuka na kusema anamuachia Mwenyezi Mungu kama huo aliousema Mama Diamond ndiyo ukweli.

 

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA na magazeti mengine Pendwa ya Global Publishers, yalishaandika kuhusiana na habari hii kabla hata Mama Diamond hajaiweka hadharani.Magazeti Pendwa yaliripoti juu ya kuwepo kwa Baba Diamond mwingine tofauti na Abdul Juma ambaye tayari alishafariki dunia miaka mingi iliyopita.

Pamoja na hilo, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linafahamu, Diamond alishaelezwa ukweli kuwa, Abdul Juma siyo baba yake na mama yake na ndiyo maana alikuwa kimya licha ya ‘kelele’ za kumtaka amsaidie mzazi wake kuwa nyingi.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

4 Comments

 1. SASA BASI, Baba wa Huyu mtoto wa Kiume mvaa kikuku ni Mzee Mrisho. (Ubuyu wa rangi ya Waridi)
  Na Mimba iliingia huko kwao Nyakabiga (Bujumbura) hapo ni baada ya kukosa soko Kigoma.
  Uchangu Doa Soko lilikuwa bado halina Kasi.

  Babake yuko Kahama. Tena wamefaana kopi pesti

  Kweli Esma na Lokole mmeamua kumuumbua Sanura na kuweka kitabu chake hazalani bila Huruma..??
  mtamuua Sanura kwa Aibu na Plesha.

  Mzee Mrisho nae anadai mtoto..!! Yamewafika msio yategemea. Kesi Aibu Heshima Umalaya vyote vimechanganyika.

  Mwana Hawa ndio haelewi wala kujitaambua. DUNIA HAADAA ULIMWENGU...(Yetu Macho na Ndewe)

  ReplyDelete
 2. Basi ukweli wenyewe, Baba wa Huyu mtoto wa Kiume mvaa kikuku ni Mzee Mrisho. (Ubuyu wa rangi ya Waridi)
  Na Mimba iliingia huko kwao Nyakabiga (Bujumbura) hapo ni baada ya kukosa soko Kigoma.
  Uchangu Doa Soko lilikuwa bado halina Kasi.

  Babake yuko Kahama. Tena wamefaana kopi pesti

  Kweli Esma na Lokole mmeamua kumuumbua Sanura na kuweka kitabu chake hazalani bila Huruma..??
  mtamuua Sanura kwa Aibu na Plesha.

  Mzee Mrisho nae anadai mtoto..!! Yamewafika msio yategemea. Kesi Aibu Heshima Umalaya vyote vimechanganyika.

  Mwana Hawa ndio haelewi wala kujitaambua. DUNIA HAADAA ULIMWENGU...(Yetu Macho na Ndewe)

  ReplyDelete
 3. Mhhhh. Makubwa.

  Asie na Mwana aeleke jiwe, tigite.

  ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)