Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Esma, Queen Darleen Kama Zamani


DAR: Zile taarifa zilizosambaa hivi karibuni mitandoani kuwa ndugu wawili wanaounganishwa na nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Esma Khan na Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, hawaivi chungu kimoja, hatimaye zimeisha.

 

Taarifa ikufikie kwamba, Esma na Darleen, sasa mambo ni kama zamani kama vile hakuna kilichotokea kati yao.

 

Sekeseke hilo limeisha mapema wiki hii, baada ya Esma kuposti picha ya pamoja akiwa na Darleen katika akaunti yake ya Instagram na kusindikiza na maneno yaliyoashiria wana kipindi chao cha runingani kitakachokuwa kinaonesha maisha yao halisi (reality show) na kuwafanya wananzengo kubaki midomo wazi.

 

“Ila hawa wadada mmh! Acha nikae kimya tu, reality show yetu soon au tuache hiihii ya Insta?” Esma alimuuliza Darleen ambapo naye kwa madai akamjibu hivi;

“(emoji za kucheka) acha tuwawekee Wasafi TV maana Insta hatupati pesa wala wadhamini!”

 

Baada ya kuona ushoga umerudi kama zamani, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Esma mwenyewe ili azungumzie ishu hiyo bila mafanikio, lakini likabahatika kumpata Darleen ambaye alijibu kwa kifupi kuwa hajawahi kuwa na tatizo na ndugu yake huyo.

 

“Kwani mimi na Esma tulikosana lini? Sisi wenyewe tulikuwa tunashangaa watu wanavyosema kuwa hatupo sawa, wakati tupo sawa, tuacheni jamani kwani watu hawawezi kuongelea watu wengine zaidi ya familia yetu?” Anahoji Darleen ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto wa kwanza kwa mumewe, Isihaka Mtoro.

 

Hivi karibuni ziliibuka tetesi kwamba wawili hao ni paka na panya baada ya kusemekana kuwa aliyekuwa mume wa Esma, Yahaya Msizwa ameshawahi kuwa sponsa wa Darleen ndiyo maana Esma hakuweza hata kuhudhuria baadhi ya shughuli za Darleen ikiwemo arobaini ya mtoto wake, Balqis iliyofanyika miezi kadhaa iliyopita maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, walikokuwa wanaishi kabla ya mambo kuharibika hivi karibuni na kuhamia Kimara jijini Dar.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments