EU, Amnesty International wataka Bobi Wine aachiwe huru wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Umoja wa Ulaya (EU) umesema ina wasiwasi juu ya wanasiasa pamoja na washika dau wa mashirika ya kiraia wanavyonyanyaswa nchini Uganda.

Taarifa kutoka kwa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Ulaya imesema vitendo vya vikosi vya usalama ambavyo havikubaliki vilisababisha vurugu kabla ya uchaguzi.


Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa serikali ya Uganda kuzuia vikosi vyake vya usalama, kuchunguza unyanyasaji na kuwajibisha wote waliokiuka hatia.


Wakati huohuo, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa mamlaka za Uganda kuagiza polisi na wanajeshi wake kuondoka mara moja katika makazi ya mgombea wa upinzani Bobi Wine ambayo wamekuwa wakiyazingira na kumzuia Bobi Wine pamoja na mke wake Barbara Itungo Kyagulanyi kutotoka nje.


‘’Huku ni kukamata watu kiholela’’, Shirika la Amnesty International limesema ikiwa ni siku saba tangu Bobi Wine na mke wake wazuiliwe kutoka nje ya makazi yao.


Robert Kyagulanyi na mke wake Barbara wamewekewa kifungo cha nyumbani bila kujulishwa makosa yao wala kufikishwa mahakamani.


‘’Kuzuiwa kwake kumefanya iwe changamoto kwa Bobi Wine kupinga matokeo ya uchaguzi katika kile ambacho kimejitokeza kuwa njama za kukizuia chama cha NUP kufika mahakamani kwa wakati,” amesema Deprose Muchena, Mkurugenzi wa Amnesty International eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika.


''Sio uhalifu kusimama kama mgombea urais wala kutaka kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani. Kuendelea kuzuiliwa kunachochewa kisiasa na ni ukiukaji wa haki za binadamu. Ni lazima kuondolewe mara moja na bila ya masharti yoyote,” Shirika la Amnesty International limesema.


Polisi wamekuwa wakimzuia Bobi Wine kuondoka nyumbani kwake tangu Ijumaa baada ya kuanza kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Januari 14.


Rais Yoweri Museveni alitangazwa mshindi baada ya kuibuka na asilimia 58.64 ya kura zilizopigwa huku Bobi Wine ambaye ndio mpinzani wake mkuu akipata asilimia 34.83 ya kura.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usalama wa Mganda, Ni jukumu la Serikali ya Uganda.
    Msitufundishe nini cha kufanya. Tutaendelea kumpatia ulinzi stahiki kulinda maisha yake. Mpaka hali ikiwa Salama na shwari juu yake.

    ReplyDelete

Top Post Ad