Fahamu mataifa 10 barani Afrika yenye pasi zenye uwezo mkubwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwaka 2021 unapojiandaa kusafiri kwa kutumia pasi yako ya kusafiria ni vyema kujua ni wapi pasi ya nchi yako inaweza kukupeleka.

Jinsi pasi ya kusafiria ya taifa lako inavyoweza kukuingiza katika mataifa mengi bila kutumia visa ndivyo jinsi kibali hicho kilivyo na uwezo .

Kila miezi mitatu kulingana na mtandao wa BBC Pidgin, Shirika la Henley Passport Index linashirikiana na shirika la usafiri wa kimataifa IATA ili kuripoti kuhusu uwezo wa pasipoti ya kila taifa wakati wa usafiri bila kutumia visa.

Katika robo ya kwanza ya mwaka 2021 shirika hilo limetoa idadi ya mataifa 10 yalio na pasipoti zenye uwezo mkubwa barani Afrika.

Pasipoti zenye uwezo mkubwa barani Afrika

Katika orodha hiyo taifa la Sycheles ndilo lenye pasipoti yenye uwezo mkubwa barani Afrika ikiwa na uwezo wa kukuingiza katika mataifa 151 bila kutumia Visa.

Katika nafasi ya pili, ni nchi ya Mauritius ambayo kibali chake cha usafiri kinaweza kukusaidia kuingia katika mataifa 142 bila kutumia Visa.

Taifa la tatu ni lile la Afrika Kusini ambalo unapoitumia pasipoti yake inaweza kukupeleka katika mataifa 101 bila kutumia visa.

Nafasi ya nne katika orodha hiyo ni taifa la Botswana ambalo pasipoti yake inaweza kukuingiza mataifa 85 bila kutumia visa.

Mataifa mengine yenye pasipoti zinazokaribiana kwa uwezo ni pamoja na Namibia, Lesotho, Eswatini na Malawi.

Pasi ya taifa la Nigeria inaweza kukuingiza katika mataifa 46 bila kutumia visa duniani, huku ile ya Ghana ikiwa na uwezo wa kukupeleka katika mataifa 65 nayo ya Cameroon ikikusafirisha na kukuingiza katika mataifa 49 bila ya kutumia visa.

Habari za hivi karibuni kuhusu pasi kumi zenye uwezo mkubwa Afrika zinaonesha kwamba Kenya ilishuka katika orodha hiyo na kuwa nambari 11.

Pasipoti zenye uwezo mkubwa duniani

Katika miaka mitatu mfululizo pasipoti ya Japan inasalia nambari moja kama pasi yenye uwezo mkubwa dunia ikiwa na uwezo wa kukuingiza katika mataifa 191 kote duniani bila kutumia visa.

Miaka michache iliopita walikuwa wakishikilia uwezo huo sawa na Singapore.

Hatahivyo Singapore imeshuka nafasi moja chini na kuwa nambari mbili huku pasi yake ikiwa na uwezo wa kukuingiza katika mataifa 190 duniani bila kutumia visa.

Korea Kusini na Ujerumani zinashikilia nafasi ya tatu kwa pamoja.

Mataifa matatu ambayo pasipoti zao zina uwezo wa chini duniani ni Syria, Iraq na Aghanistan.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad