Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Fred Vunja Bei Awekwa Mtu Kati..Afunguka A to Z Alipolipata Jina la Vunja Bei

Fred Vunja Bei Awekwa Mtu Kati..Afunguka A to Z Alipolipata Jina la Vunja Bei

Kama bado unahangaika kupata jina la biashara basi kwa hadithi hii ya mfanyabiashara maarufu wa mavazi nchini Fred Vunjabei itakupa maarifa zaidi.


Akipiga stori kwenye 'Main Seat' ya EMPIRE kupitia @efmtanzania jana, Fred ambaye ni mmiliki wa maduka ya Vunja Bei alisema jina hilo alilipata akiwa Chalinze mara baada ya kumsikia muuza korosho mmoja akitamka jina hilo.


"Nilikuwa nataka kuanzisha biashara ya nguo lakini nilitaka jina ambalo litakuwa rahisi kwa maana ya vitu vya bei nafuu. Baada ya kuhangaika na majina kama 'Bei Chee' na mengine sikuridhika. Kuna siku nilikuwa kwenye gari napita Chalinze, nikamsikia jamaa mmoja Muuza Korosho nje akisema; 'Nunua 3 upate 1 bure, ni #VunjaBei hivyo nikalipenda hilo jina na nikaamua kupita nalo." alisema Fred.


Safari moja huanzisha nyingine, Fred anasema hakuanzia kwenye nguo, safari yake ilianza kwenye kuajiriwa kwanza. Baadaye aliamua kuacha kazi wakati akiwa kwenye nafasi ya juu kabisa (Cheo) kwenye taasisi hiyo. Alijiingiza kwenye uuzaji magari na baadaye kuanzisha biashara ya mavazi ambayo hadi leo Tanzania inamtambua kwa mafanikio yake makubwa.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments