Gari la RPC Geita lawaka MOTO kwenye ajali, mtu mmoja afariki dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Gari ya Kamanda wa polisi mkoa wa Geita na gari ndogo ya abiria aina ya Hiace leo mchana zimewaka moto na kuteketea baada ya ajali iliyosababishwa na dereva boda boda aliyekua amebeba mafuta ya dizeli.


Hata hivyo, Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Hendry Mwaibambe hakuwemo kwenye gari hiyo na amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea leo majira ya saa 8.46 mchana katika eneo la Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.


Katika ajali hiyo, dereva wa boda boda ambaye inasemekana  amepoteza maisha huku watu 16 wakijeruhiwa ambapo wawili kati yao ni askari polisi.


Akielezea tukio hilo,  Kamanda Mwaibambe amesema dereva wa boda boda huyo alikuwa amebeba lita 100 za mafuta ya dizeli akaingia barabarani bila umakini na kugongwa na gari ya kamanda kisha kwenda kugonga hiace iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara na kusababisha magari yote kuwaka moto .


Amesema gari hiyo ya polisi yenye namba PT 4447 iliyokuwa ikiendeshwa na Koplo Manase Nestory imewaka moto kufuatia cheche za pikipiki baada ya ajali kuangukia mafuta yaliyomwagika.


Kwa mujibu wa kamanda,  majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya ya Chato na kwamba hali ya dereva wa Hiace ni mbaya huku polisi wakitibiwa na kuruhusiwa kuondoka.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad