Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Hayawi Hayawi :Fainali ya KOMBE la Mapinduzi ni Yanga na Simba

 


 MABINGWA mara tatu wa Kombe la Mapinduzi Simba wanatinga hatua ya fainali baada ya kushinda mbele ya Namungo FC kwenye nusu fainali ya pili kwa ushindi wa mabao 2-1.Mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Amaan, Simba ilianza kushinda mapema dakika ya 6 kupitia kwa Meddie Kagere baada ya kiraka, Abdulhaman Humud kujichanganya wakati wa kuokoa hatari.


Bao la pili ilikuwa ni kazi ya Miraj Athuman dakika ya 39 baada ya kutumia mpira uliopigwa na kiungo Hassan Dilunga kugonga mwamba akakutana nao ukiwa unarejea uwanjani na kuuzamisha kambani.


Namungo hawakuwa wanyonge kipindi cha pili waliwapa tabu Simba ambapo dakika ya 83 Kichuya Shiza aliingia ndani ya uwanja akichukua nafasi ya Jaffary Kibaya.


Ilimchukua dakika nne kuweza kutengeneza nafasi ambapo alitoa pasi kwa kupiga faulo iliyokutana na kichwa cha Stephen Sey aliyepachika bao kwa kichwa dakika ya 87.


Simba walikuwa kwenye presha kubwa kipindi cha pili baada ya Namungo kuzinduka katka kusaka ushindi ila muda ulikamilika kwa Simba kushinda mabao 2-1.


Matokeo hayo yanaifanya Simba kutinga hatua ya fainali na inakwenda kukutana na Yanga, Jumatano. 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments