Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Hemedy PHD ‘Kumuoa’ Uwoya

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

VUTA picha! Mtoto mzuri, Irene Uwoya anaolewa na handsome boy anayefanya Bongo Fleva ambaye pia ni muigizaji Hemed Suleiman ‘Hemedy PHD’ wanaoana nini kitatokea? Itakuwa furaha na nusu si ndio…!

Basi bwana, Hemedy PHD yeye kama hilo litatokea anaonekana hana kinyongo kabisa kwani amesema ameshibana sana na mrembo huyo.

Kauli hiyo Hemedy aliitoa juzi Jumanne, wakati alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kipindi cha Kata Mbuga kinachorushwa na +255 Global Radio iliyopo Sinza Mori jijini Dar.

Mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho, alimuuliza Hemedy kuwa, endapo itatokea ameshikiwa bunduki na kuambiwa achague mwanamke wa kumuoa kati ya Uwoya, Wolper na Wema, hakupoteza muda, fasta tu akamtaja Uwoya.

“Nitamchagua Uwoya,” alisema Hemedy.

Alipoulizwa kwa nini Uwoya na si hao wengine, Hemedy alisema amemchagua huyo sababu wameshibana.

“Uwoya ni mtu ambaye tumeshibana sana na tunaheshimiana kuliko kitu chochote, kila mara huwa naongea naye pia popote alipo kama ananisikia namwamwambia nampenda sana.

Mara ya mwisho tulionana juzi tu hapa kwenye bethidei yake,” alisemaa Hemedy.

Hata hivyo, Hemedy alisema pia yeye na Wema ni marafiki wa karibu na amekuwa akishirikiana naye zaidi kwenye kazi zake za sanaa.

Alisema Wema ameshakiri kuwa kati ya waigizaji watatu anaowakubali, Hemedy lazima awepo.


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

1 Comments

  1. Wopa walizinguana katika mgao wa dili la deni. lakini poa
    yote tisa, Itakuwa Hapatoshi Na Mama TAUSI akisaidiwa na super staa wetu Dada Dorah.nikombioni kumuona Pierre likwidi

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)