Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Inatisha! Kijana Awaua Baba, Dada… Naye Auawa
MCHUNGAJI wa kanisa wilayani Nyamagana, jijini Mwanza na binti yake wameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu na mtoto wake wa kiume ambaye naye alifariki baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira.

 

Mchungaji huyo wa Kanisa la Yesu Nakupenda Umeokoka, Beneth Karange (66) na binti yake Renatha Beneth (42), waliuawa juzi majira ya saa tisa alasiri.

 

Anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo ni kijana wake wa kiume, Richmond Beneth, ambaye naye alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Sekou Toure kutokana na kupigwa na wananchi wenye hasira.

 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Murilo Jumanne, alisema Richmond (32), alikuwa akisoma Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo jijini Dar es Salaam.

 

Kamanda Muliro alisema, kijana huyo ambaye naye aliuawa, aliwachoma kisu baba na dada yake sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha vifo vyao papohapo. Muliro alisema kijana huyo aliyesababisha mauaji hayo, alirudi nyumbani kutoka chuoni kwa kukosa ada.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments