Jafo atangaza wiki nzima ya kupiga nyungu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, ametangaza siku saba za kupiga nyungu kwa Watanzania huku wakiendelea kumuomba Mungu, alizozipa jina la 'One week season Three' ili watu wajifukize huku wakiendelea kuchapa kazi na Corona ikose nafasi.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 30, 2021, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora mara baada ya Rais Dkt. John Magufuli, kumaliza kuweka jiwe la msingi katika jengo la wagonjwa wa dharura katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora pamoja kuzindua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda maeneo ya Tabora, Nzega na Igunga.

"Hapa Corona haina nafasi, Mh Rais tutaendelea kumuomba Mungu kama ulivyoelekeza na umesema watu wajifukize sana na Rais naomba nikuambie Jumatatu tunaanza kampeni nyingine ya one week season three, nyungu kama kawaida tunajifukiza, tunakula matunda tunaanza tarehe 1 hadi tarehe 7 hatupoi kazi inaendelea, uchumi wetu lazima usimame", amesema Waziri Jafo

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yes...!!! Watanzania tuitikie mwito huu kwa Nguvu.
    Tunahitaji NYUNGU na Hata Watalii walioko nchini ndio haswaa.

    Nyungu kwa sasa ni wakati mufaka. na kinga zote kuzingatiwa.
    Na tuzidi kumuomba Mungu, Muwezawa yote.

    ReplyDelete

Top Post Ad