1/25/2021

JPM Aanika Alichozungumza na Rais wa Ethiopia 

RAIS  John Magufuli amempokea mgeni wake Rais wa  Ethiopia, Sahle-Work Zewde, aliyewasili nchini leo Januari 25, 2021, kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

 

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita, Magufuli amesema Tanzania na Ethiopia zina uhusiano mzuri tangu wakati wa kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika na harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, kama ambapo waasisi wa mataifa hayo hayati Mwalimu Julius Nyerere na Haile Selassie walivyokuwa mstari wa mbele.

 

 

Magufuli ameongeza kuwa, kutokana na ushrikiano huo, biashara kati nchi hizo imeanza kuimarika, mwaka 2016 ambapo biashara ilikuwa sh. bilioni 3.07, na 2019/2020 imefikisa sh. bil. 3.55 na Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania, kimesajili miradi 13 kutoka Ethiopia.

 

“Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimesajili miradi 13 kutoka Ethiopia yenye thamani ya Dola milioni 14.57 ambazo zimetoa ajira 677, tunashirikiana kwenye Sekta ya Usafiri wa Anga na Utalii, Marubani wa Tanzania 75 na Wahandisi wa Ndege 20 wamepata masomo Ethiopia.

 

“Tumezungumza masuala mengi, ikiwa ni pamoja na kunipongeza kwa kuchaguliwa kwangu kuwa rais kwa kipindi cha pili, pia  ameshukuru mahusiano yaliyopo kati yetu na bahati nzuri Ethiopia uchumi wake uko juu nafikiri unaongoza Afrika.

 

 

“Nimemueleza kwamba tuna wafungwa wapatao 1,789 kutoka Ethiopia ambao waliingia nchini kwa njia isiyo halali, tumezungumza namna ya kuwaruhusu warudi na nimemwambia hatuna masharti yoyote na kwa kuzingatia undugu tunawaruhusu waondoke free (bila ya masharti).

 

“Rais Sahle amekubali wataenda kujadili ili wafungwa 1,789 wa Ethiopia ambao wamehukumiwa Tanzania warudi kwao wakasaidie kujenga uchumi, kwa vile wana ndege nimemshauri wanaweza kuleta ndege ikawachukua, na hatuna masharti hata waliofungwa leo tutawaachia.

 

 

“Tanzania na Ethiopia zinajadiliana kuhusu ushirikiano kati ya majeshi na kuanzisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa.

 

“Ethiopia ni nchi inayoongoza kwa mifugo sisi ni wa pili, wao  wamenufaika na mifugo yao, wanatengeneza mabegi, mikanda n.k, na wana soko kubwa Ulaya, sisi bado haijatupa faida, tumekubaliana wakaribishe wawekezaji na pia sisi tukajifunze kwao.

 

 

“Nimemwomba Rais Sahle kuhusu kiwanja chetu kule Ethiopia ambacho tulichelewa kujenga, kwani hela tulizopeleka zililiwa na balozi wetu huko (sio huyu anayekaimu), tukamrudisha nyumbani.  Sheria za kule  ni kwamba kiwanja ukipewa na usikiendeleze unanyang’anywa, tumemwomba rais aturudishie.

 

 

“Rais Sahle angependa sana kulala hapa, anasema siku nyingine akija atakuja alale,  na mimi nimemkaribisha. Tuna Wambulu na Wairaki hapa ambao walitoka Ethiopia, nimemtolea mfano kwamba Sumaye ambaye amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka kumi ni Muiraki na hata wanafanana na Waethiopia,” amesema Magufuli.

 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger