Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kaze: Yanga Itabeba Kombe la MapinduziKOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema kuwa ana matumaini makubwa kuwa kikosi chake kitatwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi licha ya ushindani mkubwa ambao umekuwa ukionekana kwenye michuano hiyo.

 

Yanga imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itakayopigwa leo baada ya kujikusanyia pointi nne kwenye michezo yake miwili ya Kundi A ambapo ilishinda dhidi ya Namungo na kutoa sare dhidi ya Jamhuri.Akizungumza na Championi Jumatatu,Kaze alisema: “Tumefika hatua ya nusu fainali, nawapongeza vijana wangu kwa kupambana kwa kuwa ni wazi kumekuwa na ushindani mkubwa miongoni mwa timu shiriki.“Tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapata matokeo chanya kwenye mchezo wa nusu fainali ili kukata tiketi ya kucheza hatua ya fainali.“

 

Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda ubingwa wa michuano hii ili kuzidisha morali ya kufanya vizuri zaidi pale tutakaporejea kwenye mzunguko wa pili wa ligi.”

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments