Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kiungo Platinum: Nakuja Simba SCNOMORE Chinyerere kiungo kiraka wa FC Platinum ya Zimbabwe amesema kuwa yuko tayari kuja kucheza Simba ambayo inaelezwa imemuwekea dau mezani.

 

Awali chanzo kutoka ndani ya FC Platinum kililiambia Championi Jumamosi kuwa, Simba ilimfuata kiungo huyo mapema baada ya kumaliza mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ili waweze kupata saini yake baada ya kuvutiwa na uwezo wake.

“Viongozi wa Simba walikuja na kuuliza bei yake kuhusu mchezaji wetu ila kwa kuwa viongozi walikuwa na mchezo wa marudio waliwachunia. Kwa sasa kazi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika imeisha hivyo ni wakati wa kukaa chini kuzungumzia dili hilo,” kilisema chanzo hicho.

 

Hata hivyo, Championi Jumamosi lilimtafuta Chinyerere ambaye alikuwa kwenye kikosi cha Platinum kilichopoteza kwa kufungwa mabao 4-0 na Simba pale Uwanja wa Mkapa ili aweze kuthibitisha suala hilo ambapo alikiri kufahamu kuhusiana na kuhitajika Simba.“

 

Nimesikia kuhusu kuhitajika ndani ya timu nyingi za hapa Tanzania, nikiwa mchezaji nipo tayari kucheza na ninajua zipo timu nyingi ambazo zinatajwa kuhitaji saini yangu ikiwa ni pamoja na Simba, mimi sioni tabu nitacheza bila mashaka yoyote,” alisema Chinyerere.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments