Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

KIUNGO wa Simba, Luis Miquissone kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo anatajwa kuzivutia timu nyingi ndani ya Afrika ambazo zinahitaji kupata saini yake.
Luis amekuwa imara ndani ya Simba baada ya kuibuka kwenye dirisha dogo Januari 2019/20 akitokea Klabu ya UD Songo ambapo alionekana na mabosi wa Simba baada ya kuitungua timu hiyo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya awali.

Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuiwinda saini yake ni pamoja na Klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe inayonolewa na Kocha Mkuu, Norman Mapeza.

Mapeza alikutana na balaa la Luis Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe wakati timu yake ikishinda kwa bao 1-0 na ule wa marudio Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda mabao 4-0.

Denzil Mnkandla, meneja wa wachezaji ndani ya Klabu ya FC Platinum ameweka wazi kwamba miongoni mwa wachezaji ambao wamevutiwa naye ni pamoja na Luis.

"Sisi tuna wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja ila kwa namna ambavyo tumekitazama kikosi cha Simba kuna mmoja ambaye ana uwezo mkubwa tungependa kupata saini yake ni Luis.

"Kijana yupo vizuri ndani ya uwanja na nje ya uwanja ukimuona yupo kawaida sana ila ana uwezo mkubwa hilo lipo wazi," amesema.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Luis ametoa pasi moja ya bao ilikuwa kwenye mchezo wa awali dhidi ya Plateau United ya Nigeria na aliwapa tabu pia Uwanja wa Mkapa.

Pia Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe Simba ilishinda

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments