Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kumbe Mkali Wenu ni Ticha!MSANII wa vichekesho anayefanya poa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii, Jackson Supakila Miraji ‘Mkali Wenu’ amesema kuwa ukiachilia mbali na kazi ya uchekeshaji pia yeye ni mwalimu wa sekondari.

Akizungumza na AMANI, Mkali Wao ambaye kwa sasa anatikisa kwa uchekeshaji wake wa uchambuzi wa masuala ya mastaa wa Bongo Instagram, amesema kuwa watu huwa wanamchukulia kama hajielewi ila wanatakiwa kutambua yeye ni mtu mwenye wadhifa wake.

“Watu wakiniona Instagram na lile shati langu la kitenge wanadhani kama sina akili mimi najielewa sana tu, yote haya nafanya kwa ajili ya kujitafutia riziki, unajua watu hawawezi kuamini kwamba mimi ni mwalimu wa sekondari kabisa,” alisema Mkali Wenu.

Mbali na hilo msanii huyo ameeleza kuwa mafanikio aliyoyapata kwenye fani yake kupitia sanaa hiyo mwaka 2020 ni pamoja na kuweza kujenga nyumba na kununua gari.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments