Maalim Seif Afunguka Ukweli Mchungu "Mivutano ya Kisiasa Inaathiri USTAWI wa Zanzibar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Maalim Self Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa #Zanzibar, akiwa kwenye ziara Mkoa wa Kusini Pemba amesema, mivutano ya kisiasa imekuwa ikiathiri ustawi wa Zanzibar


Amesema, “Sisi sote tuna maslahi mapana na hatma ya Zanzibar, na kama maslahi yakiwa mazuri sote tutanufaika, na maslahi yakiwa mabaya basi sote tutaathirika, hivyo lazima tutambue sisi ni ndugu na Zanzibar ndio nyumbani kwetu"


Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, suala la ushirikiano katika nchi haliepukiki na Zanzibar inahitaji umoja na mshikamano. Uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, unaonesha maendeleo ya Zanzibar yataletwa na Wazanzibar wenyewe


Ameongeza, “Uchaguzi Mkuu umeacha majeraha makubwa kwa Wananchi na hii imetokea baada ya kutokuwepo ushirikiano. Mbali na yote yaliyotokea, mimi na Rais Husein Mwinyi, tumesafiana nia na lengo letu kwa sasa ni kujenga Nchi hii, kuweka umoja na mshikamano kwa maslahi yetu na vizazi vyetu”.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Allah, akuhifadhini nyote. na kama alivyo tuamuru.
    Shikamanenni na mShike kamba ya mwenyezi mungu na mafanikio yenu/yetu tutayaona na kuyafrahikia.

    Hussein/Maalim.. Yalopita yamepita tuko wamoja. na inshallah tutaendelea kuwa wamoja.

    Kuyaondoa machungu ni Wajibu wetu sote, na kuwarudisha washikiliwa kwa familia zao pia tulishughulikie mapema na Allah atatulipa kwa Jazaa ya Kheri.

    ReplyDelete

Top Post Ad