Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mabosi Yanga wajipange kuvunja benki kumpata Clatous Chama
IKIWA mabosi wa Yanga bado wapo kwenye hesabu za kupata saini ya nyota wa Simba, Clatous Chama inabidi wajipange kuvunja benki kuipata saini ya nyota huyo.
Awali ilikuwa inaelezwa kuwa mwamba huyo mwenye tuzo ya mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/21 yupo kwenye rada za watani hao wa jadi.

Msimu wa 2019/20 alifunga mabao mawili ndani ya Simba na kutoa pasi 10 za mabao pia jina lake lilikuwa kwenye orodha ya kikosi bora  na tuzo nyingine aliyosepa nayo ni ile ya kiungo bora.

Tayari Chama ambaye mkataba wake ulikuwa unameguka msimu huu na alikuwa huru kuzungumza na timu nyingine ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Simba.

Hivyo kwa timu ambazo zimevutiwa naye ni muda wa kukaa mezani na Simba ili kujua namna gani wanaweza kuvunja mkataba.

Nyota huyo ameongeza dili la miaka mitatu kubaki ndani ya Klabu hiyo ambayo ipo chini ya Kaimu Kocha, Seleman Matola.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments