1/29/2021

Magufuli aelezea alivyotaka kumfukuza Waziri wake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amempongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso, kwa kuchukua maamuzi ya kuwafukuza wakandarasi feki wa mradi wa maji uliopo Mwanga na kumweleza kuwa kama angechelewa basi angemfukuza yeye.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 29, 2021, wakati akizindua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria wa Kagongwa hadi Isaka mkoani Shinyanga, ambapo amewataka viongozi wahakikishe miradi yote wanayoisimamia haikwami na ikiwezekana ikamilike kabla ya muda.


"Watanzania wamechoka kusubiri miradi, nataka miradi ikamilike mapema na isiwe inazaa variation, nimeshukuru umeanza kuchukua hatua kwa wakandarasi feki waliokuwa kule Mwanga ukawafukuza kwa sababu ungechelewa kuwafukuza mimi ningekufukuza wewe ni vizuri wale wanaokuchelewesha wewe fukuza tu", amesema Rais Dkt. Magufuli.


"Pia wale wakandarasi uliowafukuza, zungumza na bodi ya wakandarasi wafutwe na wasipate kazi yoyote Tanzania kwa vile tuna ushirikiano wa Nchi za Jumuiya ya Umoja wa Afrika Mashariki peleka majina yao kule hatuhitaji wakandarasi matapeli, Waziri umeanza vizuri na moto ulioanza nao endelea nao, usicheke na hawa wakandarasi cheka na maji unapokuwa unayanywa", ameongeza Rais Magufuli

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

 1. Cheka na Maji unapokuwa Unakunnywa.

  Hiyo ni meseji kubwa na Nzito kwa Wateuliwa Wote katika nafasi zao.

  Wenye kujielewa wameielewa. JPM is a +Ve RESULT ORIENTED PRESIDENT.
  NO nonsense .

  YOU ARE INN, IF YOU DO, AND YOU ARE OUT IF YOU DONT.

  Baba JPM nakuvulia kofia. hamna kubembelezana. Performance matters.
  AFRICA NEEDS YOU AND LIKE YOUTO DRIVE IT.

  Allah Aendelee kukupa Afya njema ututumikie zaidi.

  MLUNGU AKUTAZE MWAHA,, MILIMO YAKO MISWANOO SANA. ZWALIL'II TWAIONAA.

  ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger