Mahakama Yathibitisha Kifungo cha Miaka 20 kwa Rais wa Zamani wa Korea Kusini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahakama Yathibitisha Kifungo cha Miaka 20 kwa Rais wa Zamani wa Korea Kusini

Mahakama ya juu ya Korea Kusini leo imethibitisha adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela, kinachomkabili rais wa zamani Park Geun Hye. 


Mahakama hiyo imesema inakataa rufaa iliyowasilishwa na waendesha mashitaka dhidi ya muda uliopunguzwa wa adhabu ya kifungo gerezani uliotolewa mwezi Julai. 


Hukumu hiyo inahitimisha uamuzi wa mwisho wa mashitaka ya ufisadi dhidi ya rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 68. 


Park anashitakiwa kwa makosa ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka, sambamba na hongo katika mashitaka mengine kufuatia kashfa ya mwaka 2017 iliyosababisha kuondolewa madarakni. 


Park ambaye ni binti wa dikteta wa kijeshi Park Chung Hee, aliondolewa madarakani kufuatia wiki kadhaa za maandamano yaliyomtaka ajiuzulu. 


Kiongozi huyo mara zote amekana mashitaka dhidi yake akisema anaandamwa kisiasa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad