Makala Kumzawadia Milioni Moja Atayembaini Anayeharibu Mabomba ya maji

advertise here

 DIWANI wa Kata ya Magindu Erasto Makala, amesema kuwa atamzawadia mkazi yeyote atayemkamata mtu anayehujumu miundombinu ya maji katani humo.


Makala ametoa kauli hiyo akizungumza na Waandishi wa habari Magindu, hatua inayolenga kulindwa miundombonu hiyo mbapo alisema kwamba lengo iweze kuwa endelevu huku ikiwapatia wana-Magindu huduma ya maji.


Alisema kuwa kwa sasa wakazi hao wanapata maji kupitia mradi wa DAWASA unaotoa maji kutoka chanzo chake cha Wami, ambapo kumekuwa na upoteaji wa maji njiani hali inayochangiwa na kuharibiwa kwa mabomba.


"Serikali inatupatia huduma muhimu wananchi wake ikiwemo barabara, maji, umeme, afya na elimu, lakini kuna baadhi yetu tunahujumu miundombinu husika, nitampatia kitita cha shilingi milioni moja mtu atayembaini anayehujumu miundombonu hiyo," alisema Makala.


Aliongeza kuwa Serikali kuanzia ya awamu ya kwanza mpaka hii ya tano imefanya juhudi kubwa za kuwapatia wananchi wake huduma mbalimbali, lakini kuna baadhi yao wanafanya hujuma katika baadhi ya miradi hiyo, hivyo ndani ya Kata yake hatokubali yatokee.

Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako Kirahisi


Aidha aliwataka wakazi wa vijiji vinavyounda Kata hiyo kuyatunza malambo yanayotumika maeneo yao, kwani panapotokea maji kukosekana wananufaika na malambo hayo hivyo ni vema wakayatunza vizuri ili yaendelee kuwapatia huduma.


"Ingawa kwa sasa tunapata maji ya DAWASA kupitoa mradi wake wa Wami, lakini pia ni vema tukayatunza malambo yetu kwani kwa miaka mingi yamekuwa msaada mkubwa kwetu, hivyo ni vema tukayatunza ili yaendelee kututunza," alimalizia Makala.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE