Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Makubwa! Eti Zari Amweka Mama D Kiganjani

 


SUPASTAA wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaringa mwenyewe na watoto wake wane aliozaa na wanawake watatu tofauti kisha akatengana nao.

 

Kinachokuwa kimebaki ni kuhakikisha Diamond au Mondi anawahudumia watoto wake, lakini kwa siku za hivi karibuni, mmoja wa mababy-mama wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, inasemekana ana jambo lake.

 

Zari kwa sasa yupo karibu mno na familia ya Mondi hasa mama mzazi wa jamaa huyo, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’, kiasi cha baadhi ya watu kudai kwamba amemweka kiganjani mkwe wake huyo.


Zari ambaye ni raia wa Uganda mwenye maskani yake pale Durban nchini Afrika Kusini amezaa watoto wawili na Mondi, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

 

Zari ndiye mwanamke aliyeishi na Mondi kwa muda mrefu zaidi ukilinganisha na mwanamitindo Hamisa Mobeto na Tanasha Donna.


Zari alipotimba Bongo mwishoni mwa mwaka jana, alikaribishwa kwa bashasha mno kuanzia yale mapokezi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar hadi nyumbani kwa Mondi ambako alikaribishwa kama mama mwenye nyumba.

 

Kubwa kuliko ni namna alivyopokelewa na Mama Dangote ambaye baadhi ya watu waliamini ana ugomvi naye hivyo hawezi kumkaribisha tena kwenye familia yake.

 

Lakini tofauti na matarajio ya wengi, wawili hao walishuhudiwa wakifurahiana na kutumia muda wao mwingi kufurahi pamoja, wakienda sokoni, wakipika, kuzungumza na hata kucheza muziki pamoja.


Katika posti zao za hivi karibuni, Zari alimmwagia Mama Dangote sifa tele alipoposti picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na gauni refu la rangi nyeupe.

 

Watu wengi wameishia kuweka maoni yao wakiongozwa na Zari mwenyewe katika kummwagia sifa kedekede mama mkwe wake huyo.


“Miss world of the pope…” aliandika Zari akimsifia Mama Dangote.


Naye akamjibu; “No one else!”


Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya familia ya Mondi, kwa sasa Mama Dangote humuambii kitu kwa Zari ambapo wamekuwa na ukaribu wa kutosha.


STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments