Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Marekani inasema wavamizi wa bunge walinuia kuwateka na kuwauwa wabungeWaendesha mashtaka nchini Marekani sasa wanasema waandamanaji waliolivamia bunge wiki iliyopita walikuwa wanataka "kuwateka na kuwauwa" wabunge. 
Waendesha mashtaka hao wameyasema hayo katika kesi ambayo walikuwa wanamtaka jaji mmoja aendelee kuwazuia Jacob Chansley kutoka Arizona na mtu aliyepigwa picha akiwa amejivalisha pembe akiwa katika afisi ya Makamu wa Rais Mike Pence katika bunge la seneti wakati wa uvamizi huo. 

Mawakili wa idara ya sheria kutoka Arizona walielezea kwa kina kuhusiana na uchunguzi wa idara ya upelelezi Marekani FBI kumhusu Chansley wakisema aliwacha ujumbe kwa Pence akimwambia, ni suala la muda tu kabla haki kupatikana. Chansley anatarajiwa kufikishwa mahakamani baadae leo. 

Idara ya sheria Marekani imewafungulia mashtaka zaidi ya watu 80 kuhusiana na uvamizi huo uliofanyika Jumatano iliyopita.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments