1/15/2021

Mbwana Samatta Arejea Kikosini na Balaaa...Atundika BaoMSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, Mbwana Samatta amerejea rasmi Uwanjani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu na kutupia bao kwenye mchezo dhidi ya Kasimpasa.

Samatta alifunga bao hilo dakika ya 51 ya mchezo huo wa Turkish Cup raundi ya 16 uliopigwa kwenye Uwanja wa Şükrü Saracoğlu, ambapo alianza kwenye kikosi cha kwanza kabla ya kutolewa dakika ya 69 na nafasi yake kuchukuliwa na Ozan Tufan.


Samatta amekuwa nje ya Uwanja tangu mwezi Novemba mwaka jana kutokana na majeraha ya misuli ambayo yalimfanya akose michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON ambapo Taifa Stars ilipepetana dhidi ya Tunisia Novemba 13, na 17.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger