Michael B. Jordan amethibitisha kuwa na mahusiano na Lori Harvey

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Baada ya miezi kadhaa ya tetesi , sasa mchezaji filamu maarufu wa Marekani Michael B. Jordan amethibitisha kuwa na mahusiano na Lori Harvey.
Wawili hao wamezungumzia kuhusu mapenzi yao, kupitia kurasa zao rasmi za Instagram Jumapili, huku wakishirikisha umma picha za mapenzi yao katika ukurasa huo wa Instagram.

Jordan, ambaye amekuwa msiri kuhusu maisha yake ya mapenzi, alikuwa wa kwanza kushirikisha umma picha yao kwenye Instagram.

Mchezaji filamu Michael Jordan B. mwenye umri wa miaka 33 alionekana katika picha moja ya snap na Harvey, kabla ya kuonesha akimbusu. Alimshirikisha Harvey picha hizo, pamoja na mpigapicha Leo Volcy.

Harvey – ambaye aliasiliwa na Steve Harvey baada ya kumuoa mama yake 2007 Marjorie Bridges – alishirikisha umma picha hizo akiwa na Michael Jordan B. dakika chache tu baadae.

Lori ni mwanamitindo na amekuwa akionesha mitindo ya Dolce and Gabbana, katika wiki za mitindo za Paris na Milan.

Watu maarufu akiwemo mcheza filamu Gabrielle Union na mwanamuzki wa rap eyana Taylor, walituma jumbe zao kuonesha upendo wao kwa wapenzi wao.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad