Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Miili ya wagonjwa wa Covid-19 yachomwa moto Sri Lanka


Kiongozi wa Baraza la Waislamu wa Sri Lanka na mwanachama wa bunge Rauff Hakim, alisema kuwa uteketezaji wa miili ya wahanga janga la corona (Covid-19) unaleta utengano wa watu wachache wa Sri Lanka.
Rauff Hakim alitathmini zoezi la serikali ya Sri Lanka la kuchoma moto miili ya wale waliokufa kutokana na Covid-19 kwenye chumba cha maiti, huku akitoa sababu za kiafya.

Akibaini kwamba uamuzi uliotekelezwa tangu Machi 2020 ni wa kisiasa, Hakim alisema,

"Zoezi hili ni mwendelezo wa mradi wa kuchochea Waislamu walio wachache nchini. Hatua hii ilianza baada ya shambulizi la kanisa la mwaka 2019. Shambulizi lilikuwa chanzo muhimu sana kwa kutekeleza lengo la kisiasa la serikali la kuteketeza miili ya Waislamu."

Hakim alibainisha kuwa serikali ilikuwa ikijaribu kuleta hofu kwa Waislamu kwa kutumia njia ya kuteketeza miili yao bila kuzingatia msingi ya kisayansi na kusema,

"Uteketezaji wa lazima wa waathiriwa wa Covid-19 unawatenga watu wachache wa Sri Lanka na pia unasababisha uharibifu mkubwa wa kijamii."

Hanaa Singer ambaye ni Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) mjini Colombo, alimtaka Waziri Mkuu wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa "kukagua maamuzi kama haya yanayohusu janga la Covid-19" katika ujumbe wake.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments