Mikononi mwa Takukuru wakidaiwa kughushi nyaraka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara nchini Tanzania, inawashikilia Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji cha Kimotorok, Merubo Parimelo na mjumbe mstaafu wa Serikali ya kijiji hicho Daniel Melau, kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo ya kughushi nyaraka za Serikali.


Akizungumza na Mwananchi Digital leo Januari 24, 2021, Mkuu wa Takukuru Mkoani Manyara, Holle Makungu amesema watuhumiwa hao wawili wamekamatwa juzi kijiji kwao Kimotorok.

Makungu amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka za Serikali na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Amesema watuhumiwa hao walipopekuliwa majumbani kwao walikutwa na nyaraka hizo za Serikali wakiwa nazo.

“Watuhumiwa hawa wamekuwa wakizitumia nyaraka hizo za Serikali kwa kuuza ardhi ya kijiji kwa kurudisha tarehe nyuma ili kuonyesha mauzo hayo yalifanyika wakati wakiwa madarakani,” amesema.

Amedai uchunguzi zaidi umeonyesha kwamba baadhi ya wenyeviti wastaafu wa vijiji katika Wilaya ya Simanjiro huondoka na nyaraka za vijiji kwa nia ya kutenda uhalifu wa kuuza ardhi japo wameshaondoka madarakani.

Amewataka wote walioondoka na nyaraka wazirejeshe mara moja na kuzikabidhi kwa maofisa watendaji wa vijiji wanaohusika.

Amesema wasiporejesha wafahamu kuwa watakutana na mkono wa sheria kama wenzao kina Parimelo na Melau walivyokamatwa.




“Tunatarajia kuwafikisha mahakamani na kuwafungulia mashtaka ili iwe funzo kwa viongozi wote wenye tabia ya kuendelea kuhodhi nyaraka za Serikali pamoja na kustaafu nafasi zao,” amesema Makungu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad