Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mimi Mars: Vanessa Alikuwa na Kila Kitu Kwenye Muziki
UKIAMBIWA utaje listi ya warembo wanaofanya vizuri kwenye Bongo Fleva, basi nina imani kubwa kuwa hautaacha kutaja jina la mwanadada mwenye sauti nyororo ya kumtoa nyoka pangoni, Marianne Mdee ‘Mimi Mars’.

 

Ni miongoni mwa wasichana wanaofanya poa kwa ngoma zake alizofanya na zikampa jina kubwa kama Dede, Kodoo, Shuga, Haina Maana na nyinginezo.

 

UWAZI SHOWBIZ imemtafuta na kufanya naye exclusive interview ambapo amefunguka mambo mengi usiyojua;

UWAZI SHOWBIZ: Ulijisikiaje baada ya dada yako, Vanessa kutangaza kuacha muziki rasmi?

 

MIMI MARS: Nilisikitika sana kwa sababu mpaka tupate tena msichana ambaye ataweza kutufikisha tena mbali kama ilivyokuwa kwa Vee (Vanessa) itachukua muda sana, maana sasa hivi imebaki kwa wanaume tu ndiyo wanafanya vizuri kwenye gemu, japokuwa nafurahi kuona kuna wasichana ambao wanakuja kwa spidi kama Nandy, Zuchu na wengineo.

 

UWAZI SHOWBIZ: Kabla ya Vanessa kutangaza rasmi uamuzi wake huo wa kuacha muziki alikutaarifu mapema kama mtu wake wa karibu au ilikuwaje?

 

MIMI MARS: Kusema kweli haya ni maongezi ambayo yalikuwa yanatokea miaka mingi sana kabla hata mimi sijaingia kwenye gemu. Mara nyingi alikuwa analalamika tu kwamba amechoka, anatamani aache muziki, mara apumzike, lakini hatukujua kama ingekuwa hivi karibuni. Kwa hiyo nilijisikia vibaya sana; yaani amefanya mapema sana.

 

UWAZI SHOWBIZ: Unahisi uamuzi aliouchukua ni sahihi?

MIMI MARS: Unajua mtu ni bora ajikomboe mapema kuliko mwisho wa siku yakawa maji ya shingo, akazama, hivyo binafsi naona yupo sahihi, muache apumzike.

 

UWAZI SHOWBIZ: Unaposema apumzike unamaanisha nini wakati mashabiki wanajua kuwa vanessa ameacha kabisa kufanya muziki?

 

MIMI MARS: Unajua kuna kitu ambacho watu walimuelewa vibaya. Ni kwamba wanadhani ameacha kabisa, lakini ukweli ni kwamba amepumzika tu. Kwa alikuwa hataki ile ‘eeh mbona sasa umekaa sana hutoi hata nyimbo,’ sasa mawazo kama hayo ndiyo alikuwa hataki, yeye anataka akiwa tayari ndiyo atoe ngoma yake, mtaisikiliza na mtaipokea.

 

Kama ikiwa hata ni mara moja kwa mwaka, sawa, lakini kwa sasa hivi yupo kwenye mapumziko kidogo, nadhani anajipanga upya.

 

UWAZI SHOWBIZ: Haijakuathiri kitu chochote kwenye muziki maana asilimia kubwa Vanessa ndiye alikuwa akikushika mkono na kukusapoti?

MIMI MARS: Haijaniathiri kwa sababu kwa upande mwingine naweza nikasema ndiyo imenipa nafasi na sasa hivi naona watu ambao walikuwa mashabiki wake, wamehamia kwangu.

Lakini tulipokuwa wawili, watu walikuwa wanaona bora wamshabikie Vanessa, lakini sasa hivi ameniachia uwanja.

 

UWAZI SHOWBIZ: Bado mnaongea na anakushauri nini cha kufanya kwenye gemu ili uweze kufika mbali?

MIMI MARS: Tunaongea sana kwa sababu yeye bado ni bosi wa Mdee Music. Kwa hiyo kabla kazi haijatoka au kitu hakijafanyika, lazima kwanza apitie na apitishe ndiyo kila kitu kitakuwa sawa.

 

UWAZI SHOWBIZ: Unahisi ni kwa nini Vanessa amekaa sana Marekani?

MIMI MARS: Nadhani ni kwa sababu ya Corona, kule kwao hawaruhusiwi kutoka, halafu huku Bongo anarudi kufanya nini wakati kule yupo na mchumba wake na anafurahia maisha? Hafanyi muziki wala nini sasa anarudi huku kufanya nini? Bora aendelee kukaa tu hukohuko.

 

UWAZI SHOWBIZ: Kuna tetesi kwamba mchumba wake, Rotimi anamtumia Vanessa kwa sasa kwenye muziki wake ili kujiingizia kipato, hili unalionaje?

MIMI MARS: Sidhani kama ni kweli, watu wanaongea kwa sababu amemtumia kama video queen kwenye wimbo wake wa Love Somebody, lakini hakuna kitu kama hicho. Rotimi anaingiza pesa zake yeye mwenyewe hata kabla hajajuana na Vanessa.

 

Hapa tuseme tu kwamba labda Vanessa alichomsaidia ni kumpatia mashabiki wa Bongo kwa sababu sidhani kama Tanzania kuna watu walikuwa wanamjua Rotimi na kama wapo, basi ni wachache, lakini siyo kweli kwamba Rotimi anamtumia Vanessa kumuingizia pesa, kwa kitu gani alichonacho Vee? Kwa sababu yeye mwenyewe kule Marekani ni mgeni ingekuwa labda hapa Tanzania sawa, tungesema Rotimi amekuja na kupewa dili f ’lani, lakini hakuna kitu kama hicho.

 

UWAZI SHOWBIZ: Unadhani ameacha pengo gani kwenye Bongo Fleva?

MIMI MARS: Ametuachia pengo kubwa sana kwa sababu katika wasichana wa Bongo Fleva ambao walikuwa wanaongoza kuipeperusha bendera ya Tanzania, Vee alikuwa mmojawao.

 

UWAZI SHOWBIZ: Kitu gani ambacho huwa unakikumbuka sana kwenye muziki wa Vanessa?

MIMI MARS: Mapigo yake bwana; yaani alikuwa akijitolea nguvu zake zote kufanya video. Ukiambiwa Vanesaa Mdee anashusha ngoma, unajua ni ngoma kwelikweli siyo ya kitoto. Ni msanii ambaye alikuwa akitangaza kuachia ngoma, unajua kabisa lazima itakuwa nzuri.

 

UWAZI SHOWBIZ: ni msanii gani wa kike ambaye unahisi akikaza buti anaweza kufikia levo za Vanessa?

MIMI MARS: Kusema kweli hiyo itakuwa ngumu kwa sababu Vanessa alikuwa na vitu vingi. Kwanza alikuwa na ubunifu, sauti nzuri, connection, mavazi, akili, aidia na pafomansi yake ilikuwa ni balaa. Niwe mkweli, mimi mwenyewe kwenye uwezo wake wa kupafomu sijafika.

 

Naongea hivi siyo kwa ubaya, wasichana wengi wanapafomu vizuri, lakini pafomansi ya Vanessa ni tofauti kabisa, ulikuwa ukiangalia utadhani upo nje. Bado wanawake wa Bongo hatujafika kwenye levo za Vee. Najua watanikasirikia wengi na watanisema, lakini ni ukweli na wao wenyewe wanajua.

 

UWAZI SHOWBIZ: Mara nyingi Vee akihojiwa anadai kuwa wewe ni msumbufu na muongeaji sana, hii imekaaje?

MIMI MARS: (anacheka) Mimi siyo msumbufu ila ni mtu ambaye akitaka kitu anakitaka na kisipokwenda vile anavyotaka, ndiyo usumbufu unapoanza; yaani ni mtu ambaye nikitaka A wewe ukaniletea B, sitakuelewa! Lakini sasa hivi najifunza, nikitaka A ukaniletea B, basi nitajitahidi tukutane katikati, tofauti na zamani ambavyo nilikuwa na msimamo wa kutaka nibaki kwenye hiyo A yangu, ila nilivyozidi kukaa kwenye industry ya muziki nimejifunza kwamba kuna mambo yanafika mahali ni lazima mkutane katikati, mkubaliane na vitu f ’lani. Kwa hiyo nimebadilika sana.

 

UWAZI SHOWBIZ: Jambo la mwisho kwa mashabiki wako ni lipi?

MIMI MARS: Nawapenda sana na naomba wakae mkao wa kupokea tamthiliya yetu mpya ambayo nimeshiriki inaitwa Jua Kali.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments