Mjamzito Ajiua na Mimba ya Miezi 9

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MWANAMKE mmoja amejinyonga kwa kutumia kanga kwenye mti wa mwembe katika kijiji cha Itununu wilayani Serengeti, kwa madai ya wivu wa mapenzi, huku akiwa na mimba ya miezi tisa.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu, alithibitisha kwamba Mkami Nyamhanga (21) alijinyonga Januari 17. 2021, kwenye mti wa mwembe uliopo shambani.

Alisema mwili wake ulionwa na watoto waliokuwa wanakwenda kuangua matunda kwenye mwembe huo na ndiyo waliotoa taarifa ya kifo hicho. Kwa mujibu wa babu wa marehemu amedai  alikuwa anamtuhumu mume wake kuwa na mpenzi mwingine.

”Asubuhi alitoka bila kuaga mpaka alipogundulika amejinyonga kwa kutumia kitanzi cha nguo ambayo alifunga kwenye tawi la mwembe na kuning’inia,”alisema na kuongeza:

“Mganga aliyefanya uchunguzi alibaini kuwa kifo chake kimetokana na kitanzi shingoni kilichosababisha mzunguko wa damu na hewa kukosekana.  Ndugu walikabidhiwa mwili kwa ajili ya kuuzika na hakuna mtu aliyekamatwa lakini uchunguzi unaendelea.’’

Mganga mfawidhi wa zahanati ya Itununu, Melick Salapioni, alilieleza Mwananchi kuwa mwanamke huyo alikuwa na mimba inayokaribia miezi tisa.


Usikubali Kupitwa na Udaku wa Mjini INSTALL App ya UDAKU Special >HAPA ili Tuwe Tunakutumia Moja Kwa Moja Kwenye Simu Yako

Alisema kutokana na mama kujiua, alikata mawasiliano ya hewa ya oksijeni kati yake na mtoto na hivyo kusababisha kichanga hicho kufa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad