Mke na mume wanavyozikabili pamoja changamoto za kazi ya daladala

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 



Inaweza kuwa jambo lisilo la kawaida kuona kondakta wa kike akipiga debe katika daladala iliyojaa abiria kwenye mitaa yenye pilikapilika nying ya Dar es Salaam.


Lakini inaweza kushangaza pale unapokuta kondakta na dereva wake ni mke na mumewe, mke akiwa ameacha kazi yake na kujiunga na kazi hiyo ya kukusanya nauli na kuita abiria.



 

Anajipenyeza katikati ya abiria kwenye basi lililojaa akiwa na sare yake ya bluu inayoning’inia katika bega moja, nywele zilizosukwa vizuri na miwani.


Huyu ni Witness Mushi mwenye umri wa miaka 36, msomi mwenye shahada ya mawasiliano aliyeacha kazi yake kumsaidia mumewe ambaye anaendesha daladala kati ya Makumbusho na Bunju.


Witness na mumewe Athuman Hatibu ( 44) wamefunga ndoa na wanaishi Bunju, Dar es Salaam.


Walikubaliana miaka mitano iliyopita kuendesha na kusimamia basi moja wakati wakiachana na mitindo ya maisha ambayo wote wawili walikuwa nayo kabla ya kufanya kazi pamoja kwenye daladala.


Witness anasema licha ya kuwa na shahada ya mawasiliano, alichagua kumsaidia mumewe kama kondakta ili kuondoa utegemezi katika mshahara wa kila mwezi.


“Haukuwa uamuzi rahisi kufanya kwa sababu niliishi maisha tofauti kabla ya kuanza kazi ya kuwa kondakta wa daladala,” anasema Witness katika mahojiano na gazeti The Citizen.



 

“Mume wangu alikuwa na malalamiko mengi juu ya makondakta waliofanya kazi huko nyuma na mengi yalikuwa juu ya nauli kidogo iliyokusanywa kila siku.


“Nilimwambia anipe siku moja ya kujifunza na kutambua vituo vyote vya daladala katika njia ya Makumbusho hadi Bunju ili baadaye aamue kama tunaweza kufanya kazi pamoja nami kama kondakta wake,” anasema.


Anabainisha kwamba mchakato wa kutambua vituo vyote vya daladala kwa majina haukuwa mgumu kama alivyofikiri ingekuwa. Ujuzi wake wa vituo vya mabasi Dar es Salaam ulimfanya ajue majina ndani ya siku moja tu.


“Mpangilio ulifanyika siku hiyo, wakati kondakta mwingine alikuwa anataja majina ya vituo nilikuwa nikikusanya nauli kutoka kwa abiria na wakati huohuo nikijifunza tofauti ya nauli kutoka kituo kimoja hadi kingine,” anasema.


Anafafanua kuwa hakujua kuwa nauli ya daladala ya Bunju kwenda Tegeta ni Sh400 na Makumbusho kwenda Bunju ni Sh750.


Witness anasema licha ya kufanya kazi chini ya mmiliki wa daladala, kazi yao katika miaka mitano iliyopita (tangu 2016) imewapa mwanga, wao pia wanajiona wakimiliki daladala lao siku moja.



 

“Kufanya kazi pamoja kumetufundisha kuwa ni bora kuwa na basi letu kwa sababu ni wakati huo tu ndiyo tutakapoweza kutumia mapato ya nauli ili kukidhi mahitaji ya familia yetu,” anaongeza.


Witness anaelezea kuwa wote huamka saa 9 usiku kila siku ili kuhakikisha wanakuwa njiani ifikapo saa 10 alfajiri, wakijiandaa kwa siku ndefu ambayo kawaida huisha saa 5 usiku baada ya mizunguko angalau 20 kila siku.


Mama huyo wa watoto wanne -- Khatibu, Rabia, Johnson na Moreen, anasema kufanya kazi na mumewe kumemsaidia kuelewa kanuni na taratibu za kufanya kazi, wakati wote waliapa kutoleta mambo ya nyumbani kazini.


“Ndoa haijakamilika kabisa bila mizozo, lakini sisi tuliahidiana kutoruhusu hali za nyumbani kuingiliana na mazingira yetu ya kazi,” anasema Witness.


Anasema wakati wowote wanapokuwa na tofauti kama wanandoa, huziweka kando wanapokuwa wakifanya kazi pamoja.


“Sisi tunaamini kuleta shida za nyumbani kazini kunaweza kupunguza baraka za Mungu na kuathiri biashara moja kwa moja,” anasema Witness.


Anasema nyumba yao mara nyingi huachwa tupu kwani watoto wake wawili wanaishi na bibi zao wakati wengine wawili wakiwa katika shule za bweni.



 

Mume wa Witness, Athuman anabainisha kwamba alianza kuona tofauti kati ya kufanya kazi na makondakta wengine na kufanya kazi na mkewe, alipomruhusu kukusanya nauli kwa mara ya kwanza.


“Tofauti inaonekana kwa urahisi kwa sababu kiasi ambacho tumekuwa tukikusanya kwa miaka mitano iliyopita ni kikubwa ukilinganisha na kiasi ambacho walikusanya makondakta wengine niliofanya nao kazi hapo awali,” anasema Athuman.


Anatoa mfano wiki chache zilizopita mkewe aliposafiri kwenda Moshi, alimchukua kwa muda mdogo wake ili kusaidia kukusanya nauli.


“Kufanya kazi na mdogo wangu kulinithibitisha kwamba hakuna mtu mwingine aliyewahi kufikisha kiwango cha mapato ya nauli za daladala kama mke wangu anapokuwa kazini,” anaelezea.


Anamsifia Witness kwa kuweka akiba na kwamba hata gari linapokuwa limekodiwa siku nzima, mkewe anajua kiwango sahihi cha pesa kinachopaswa kulipwa na watu wanaokodi daladala hilo.


Athuman anadokeza kuwa mpango wa kununua basi lao wenyewe itakuwa hatua ya kwanza ya kujiajiri kwa familia yake kwa sababu hata mtoto wao wa kwanza, Khatibu (23), pia ni dereva wa basi la shule.


“Basi ambalo tunapanga kununua litaratibiwa na sisi na kijana wetu. Kijana wangu sasa anaboresha leseni yake ya udereva, aliyonayo inamruhusu kuendesha gari za Daraja A tu,” anabainisha.


Akiwazungumzia wanandoa hao, Aisha Raziki, mkazi wa Tegeta anasema mwanamke anayefanya kazi kama kondakta wa daladala ni jasiri hasa anapokuwa na watoto lakini kwa Witness ni suala tofauti kwa kuwa ya anafanya kazi na mume wake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad