Mkude Apewa Masaa 24 Simba Atozwa Faini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KAMATI ya Nidhamu ya Klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake Suleiman Kova imetangaza Januari 23, 2021 hukumu ya kiungo wa klabu hiyo, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi kwa makossa ya utovu wa nidhamu.

 

Kwa mujibu wa Kova, haya ndiyo makossa aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya, pamoja na hukumu zake.

Mosi: Kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).

 

Mbili: Kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union.

 

Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) na kuwekwa katika kipindi cha uangaizi cha miezi sita.



Tatu: Kutoripoti kambini siku ya 26/11/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.

 

MAAGIZO
Kamati imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.

Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndanI ya mwezi mmoja.

Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad