Mnangagwa: Marekani Haina Haki ya Kuadhibu Nchi Nyingine


BAADA ya wafuasi wa Rais Trump kuvamia Bunge la Marekani, Rais wa #Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesema Taifa hilo halina haki ya kuiadhibu nchi nyingine kwa misingi ya kidemokrasia.

Zimbabwe iliwekewa vikwazo na utawala wa Trump enzi za Robert Mugabe kwa ukiukwaji wa Demokrasia, hali inayoleta ugumu kwa Wananchi. Rais huyo amempongeza Joe Biden akisema wapo tayari kushirikiana na Marekani kwa manufaa ya pande zote mbili.

Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea vikwazo Zimbabwe kwa madai ya ukosefu wa Demokrasia na kuheshimiwa #HakiZaBinadamu na vilevile kubanwa kwa vyombo vya habari.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

  1. Tumpongeze Mteule ambae makamu wake ni mwenye asili yetu
    Tunaweza kufanya nao kazi vizuri zaidi ni wasikivu.

    Tofauti na awamu hii inayoondoka.

    ReplyDelete