Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mrembo Aanika Picha Zake na Dangote, Atoboa Siri NzitoMWANAMKE mfanyakazi katika mgahawa mmoja nchini Marekani aliyejulikana kama Bea Lewis, jana (Ijumaa) habari zake zilizagaa mitandaoni akidai kwamba tajiri mmiliki viwanda wa Nigeria, Aliko Dangote, walikutana naye mara kadhaa, jambo lililomfanya abadili maisha yake kikazi na kibinafsi.


 

Lewis, ambaye alianika habari hizo katika ukurasa wake wa Instagram usiku saa sita (juzi), amejikuta akiwa na wafuasi zaidi ya 13,000.

“Nilikutana kimahaba na mtu mweusi tajiri zaidi duniani.  Aliuchana moyo wangu katika vipande 1,000.  Nilijifunza mengi kutoka kwake kuliko mtu mwingine niliyekutana naye.  Kuwasiliana na bilionea kunakufanya uuone ulimwengu katika sura tofauti,” aliandika.

 


 

Lewis anamiliki mgahawa wa Atlanta Meal Prep, ambao hutoa vyakula vya kienyeji na hutoa huduma ya  vyakula vyenye kujenga afya, ikiwa ni pamoja na kumiliki mgahawa mwingine wa Hush Dinner Club

Katika post yake iliyokuwa ikielezea matukio ya mwaka 2020, Lewis alitoa picha  akiwa na Dangote pamoja na kadi ya (Siku ya Wapendanao) Valentine’s Day iliyotumwa kwa bilionea huyo.


 

Katika ujumbe huo mrefu, Lewis alisema kukutana na tajiri mkubwa zaidi wa Afrika kulimbadili kimwili na kumfanya aanze kutumia vyakula vya mimea.

Lewis pia alidai kwamba kukutana kwake na Dangote kulibadili mtindo wa maisha yake kikazi na kumwongezea kipato katika biashara zake.


 

Akiorodhesha mafanikio yake zaidi, alisema: “Nilijipanga vizuri zaidi na hatimaye nikaweza kuachana na kazi za kila siku za upishi.  Pia nilijifunza kupenda bila kuwa na masharti…


 

“Niligundua kwamba mgahawa wenye thamani ya dola nusu milioni ulikuwa ni kitegauchumi kibaya, hivyo nilinunua miradi miwili ambayo ilianza kuniingizia faida kubwa,” alisema.

 


“Alibadili tabia yangu kikazi na uvumilivu katika mambo ninayoyafanya.  Mabadiliko hayo yalinivutia kwa watu walioniinua na kuongeza nguvu yangu kiakili na kifedha,” alisema Lewis.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments