Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mshambuliaji mpya wa Azam FC kazini tena leoMSHAMBULIAJI  wa kikosi cha Azam FC, Mpiana Monzinzi ambaye ni ingizo jipya leo anatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo wa mwisho wa Kombe la Mapinduzi hatua ya makundi.
Azam FC ambao ni wababe Kwenye historia ya kutwaa mataji ya Kombe la Mapinduzi,  leo Januari 10 watanenyana na Malindi mchezo wa mwisho.

Katika ule mchezo wa ufunguzi ambapo walitishana nguvu kwa kufungana bao 1-1 ndani ya Kundi C, Monzinzi ukiwa ni mchezo wake wa kwanza alitupia bao lake la kwanza. 

Chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina nyota huyo raia wa Congo ameanza kupewa nafasi kikosi cha Kwanza jambo linalompa nafasi ya kutimiza ahadi yake ya kutupia mabao zaidi ya 15.

Nyota huyo amesema:"Mpango wangu ni kuona kwamba ninafunga mabao mengi kwa kushirikiana na wenzangu, itakuwa kuanzia 15 na kuendelea,".

Timu itakayoshinda leo ina nafasi ya kutinga jumla hatua ya nusu fainali na ile itakayopoteza inafungashiwa virago jumla kwa kuwa nafasi ya best loser ipo mikononi mwa Namungo mwenye pointi 3 na mabao mawili hivyo anaweza kupita kwa faida ya mabao mengi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments