Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mshambuliaji Perfect Chikwende Ndani ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.Msemaji wa FC Platinum, Chido Chizondo amethibitisha taarifa za kuondoka kwa mshambuliaji Perfect Chikwende, ambaye anahusishwa na taarifa za kuwaniwa na mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC.

Chizondo akiwa kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari mjini Harare, Zimbabwe amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesafiri kuelekea Dar es salaam, Tanzania.


Hata hivyo Chizondo hajaweka wazi mshambuliaji huyo ameelekea Dar es salaam kwa mpangowa kujiunga na klabu gani, licha ya mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC kupewa kipaumbele, huku Azam FC wakihusishwa kwenye dili hilo.

“Hatuwezi kuthibitisha kuwa ni klabu gani ameenda kujiunga nayo lakini tunaweza kusema kuwa ameondoka na kwenda Tanzania,”

“Simba wameweka mezani ofa lakini pia Azam FC nao wanaonekana kuvutiwa naye, tunasubiri kuona matokeo.” Amesema Chizondo.


Ripoti zinasema Simba wapo watayari kutoa Dola 55 000 ambazo ni zaidi ya sh 127 milioni kwa ajili ya kupata huduma mshambuliaji huyo wa zamani wa Bulawayo Chiefs , lakini Azam FC nao wanatajwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumnasa nyota huyo. Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments