Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Msusi wa Michelle Obama ang'aa kuapishwa kwa Biden

 


Mke maarufu wa rais wa zamani wa Marekani, Michelle Obama juzi alisisimua ulimwengu wa mitindo wakati alipoibuka katika hafla ya kuapishwa kwa Joe Biden, akiwa na staili ya kumwaga nywele mabeni, iliyosababisha msusi wake apate kazi lukuki.

Kama wengine, Michelle, ambaye anaonekana kama mke wa milele wa rais wa Marekani (Forever First Lady of The United States, FLOTUS), alivaa suti yenye koti refu, lakini suruali ambayo mkanda wake wa rangi ya dhahabu ulifungwa juu ya tumbo, huku suruali ikiwa ya kumwaga chini, hali iliyovuta zaidi macho ya wanamitindo.

Na aliyepata sifa zaidi alikuwa mwanamitindo wake wa nywele, Yene Damtew.

"Kusema ukweli, kulikuwa na nyota kadhaa wa mitindo waliofika jengo la bunge kushuhudia tukio la kihistoria la kuapishwa kwa Rais Joe Biden na makamu wake Kamala Harris — Harris na binti wake wa kumlea wakiwemo — lakini (Michelle) aliingiza fasheni katika jengo la bunge ikiwa na herufi kubwa ya F, kwa hiyo mara zote atavalia kitu kinachovutia kuona," ameandika Dara Prat katika tovuti ya yahoo.com.

Lakini kilichovuta macho ya wengi kiasi cha kumpatia kazi msusi wake, ni staili ya nywele.

Nywele hizo zilizoonekana zimewekwa curl, ziliangukia mabegani zikiwa zimejiviringisha miduara upande mmoja.

Michelle aliingia katika hafla hiyo akiwa ameshikwa mkono na mumewe Barack Obama, huku nywele zake zilizomwagika mabegani zikitingishika kila alipopiga hatua.

Na mara moja watumiaji wa mtandao wa Twitter wakaanza kumsifu, huku neno “laid (lazwa)” likianza kusambaa na sifa zikienda kwa msusi wake.

"Ninashukuru sana kwa mapenzi mliyoonyesha, kunitaja na kunifikishia ujumbe na vikaragosi," alisema msusi huyo katika ukurasa wake wa Instagram, akishukuru watu waliomsifu kwa ustadi baada ya kuona nywele za mke huyo wa rais wa Marekani katika hafla ya juzi.

“Mmenipa furaha leo. Nashukuru sana.”

Alisema timu yake ya staili imepokea 'mafuriko' ya maombi kwa siku moja tu.

“Mimi na timu yangu tumepokea DMs na barua pepep nyingi kuhusu huduma za staili za nywele za salon ya Aesthetics,” ameandika Yamtew.

Aliacha maelekezo ya jinsi mashabiki wake wapya wanavyoweza kupata huduma hiyo.

Magazeti ya staili nayo yakazungumzia nywele hizo, yakionyesha Michelle aliiteka hafla.

Demtew aliiambia tovuti ya PopSugar kwamba staili aliyoitumia kwa Michelle aliibuni kutokana na tukio lenyewe, akisema: “Nilitaka kutengeneza muonekano mzuri ambao ungegeuza vichwa vya watu, lakini pia nilitaka staili ambayo ingedumu kwa saa kadhaa bila mimi kuwepo pembeni yake kwa ajili ya kurekebisha.”


Usikubali Kupitwa na Udaku wa Mjini INSTALL App ya UDAKU Special >>HAPA ili Tuwe Tunakutumia Moja Kwa Moja Kwenye Simu Yako

Kwa mujibu wa Elisabetta Bianchini wa yahoo.com, Msusi huyo amekuwa akifanya kazi na Michelle kwa zaidi ya miaka kumi na anasema “ananiamini kuchagua staili ambayo itavutia na namuamini kwa kuniruhusu (kutumia) baadhi ya ubunifu.”

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments