Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

"Mwana Fa na Babu tale wasitutie aibu" - DullahRais wa BongoFleva Dullah Planet amewaomba Wabunge ambao wametoka kwenye kiwanda cha muziki wa BongoFleva mpaka mjengoni Dodoma, Mwana Fa na Babu Tale kwamba wasitie aibu kwenye shughuli zao za kuwatetea wananchi na sanaa kwa ujumla.


Akiwazungumzia baada ya kupata Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020 ambapo Mwana Fa amekuwa Mbunge wa Muheza Tanga, na Babu Tale ni Mbunge wa Kusini Mashariki Morogoro, mtangazaji Dullah Planet amesema 


"Ni ushindi kwenye tasnia yetu ya muziki na sanaa kwa ujumla kwa sababu ilikuwa inaonekana sehemu ya kihuni na miyayusho lakini tumeweza kutoa nafasi ya kutoa watu kuwakilisha Bungeni"


 "Ni heshima kubwa hongera kwao natumaini wataenda kutekeleza waliyoyaahidi na wananchi wapo tayari kuwaona wakifanya kazi kazi, na sisi tunawaambia wasitutie aibu kwa wananchi  kwa sababu wanatoka kwenye upande ambao sisi tupo, tunawategemea kwenye makubwa" ameongeza Dullah Planet

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments