Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mwanafunzi wa Kenya akiri kuiua familia yake, Baba Mama na wadogo zakeMwanafunzi wa chuo kikuu nchini Kenya amekiri kwa polisi na kutoa taarifa zaidi juu ya namna alivyopanga na kuwauwa watu watano wa familia yake, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.Simon Warunge, mwenye umri wa miaka 22, ameripotiwa kuwaambia polisi kwamba alitumia chuma kumgonga mama yake, kaka yake, baba yake na binamu yake kabla ya kuwadunga visu na kuwauwa.

Mwanafunzi huyo aliwaambia polisi kuwa wazazi wake walikuwa wafuasi wa shetani na makatili, limeripoti gazeti la the Star.

Alisema kuwa walimchukia na kumsema wakati hayupo, imeripoti televisheni ya Citizen.

Madada zake wawili ambao walikuwa wamerejea shuleni walinusurika na shambulio hilo.

Mama yake alikuwa ni muuguzi wa kisaikolojia nchini Kenya, na baba yake alikuwa muuguzi nchini Marekani na alikuwa amewasili nchini Kenya kwa ajili ya sherehe za Krismasi kabla ya mauaji hayo.

Wachunguzi wamefungua uchunguzi upya kuhusiana na mauaji mengine ambayo yalitokea katika ndugu wengine wa familia hiyo.

Polisi pia wamemkamata mpenzi wa kike wa mshukiwa. Wawili hao wamefikishwa mahakani Jumatatu:

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments