1/23/2021

Mwanafunzi wa Miaka 22 Akiri Kumuua Bibi yake Kwa Kumpiga na Chuma Walipokuwa Wakipigana

 


KENYA: Mercy Wangari anashukiwa kuwa Mtuhumiwa namba moja katika mauaji ya Bibi yake (72) baada ya kukiri kumpiga na chuma walipopigana na kupelekea kifo chake papo hapo miezi mitano iliyopita


Mwanafunzi huyo anasema, Baada ya Baba yake kupoteza kazi na kushindwa kumudu mahitaji, Bibi alianza kuongelea matatizo yao kwa ndugu wengine na wanakijiji, kitendo kilichokasirisha Familia yake


Hali hiyo ilipelekea mvutano baina na Bibi na Familia, na kwa mujibu wa maelezo ya Mercy, Bibi yake pia alianza kuwa tofauti naye ikilinganishwa na ndugu zake wawili akidhani maisha ya Chuoni yanambadilisha


Mercy alitaka kujisalimisha Polisi lakini Baba yake aliamua kumuokoa kwa kusema yeye ndiye aliyemuua Mama yake. Hivi sasa, wote wawili wanashikiliwa na Polisi wanaomalizia uchunguzi wao

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger