Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mwingine Afia gesti Akiwa na Mpenzi wake

 


Mwanza. Mtu mmoja ambaye jina lake halijatambulika amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni akiwa na mwanamke anayehisiwa kuwa ni mpenzi wake.


Tukio hilo limetokea Januari 18, 2021 katika nyumba ya kulala wageni ya Fimbo Lodge iliyopo mtaa wa Kilimahewa Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.


Mmiliki wa nyumba hiyo, Christopher Lyang’ombe akizungumza na Mwananchi Digital  leo Alhamisi Januari 21, 2021 amekiri kutokea kwa tukio hilo akisisitiza watafutwe polisi kwa kuwa ndio wanaoendelea na uchunguzi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba  wanamshikilia kwa mahojiano  mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa mtu wa karibu wa marehemu na ndio alikuwa naye katika nyumba hiyo.


“Mtu anayetuhumiwa inadaiwa ni mtu wake wa siku nyingi tunamhoji tu ila upo ushahidi wa awali unaoonyesha alikuwa na matatizo ya presha,” amesema Muliro


Tukio hilo limetokea ikiwa zimepita siku tano tangu kutokea kwa tukio kama hilo ambapo mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam, David Makerege (80) alifariki dunia katika hoteli ya Mbezi Garden alipokuwa na Neema Kibaya (33).


Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhan Kingai aliwaeleza waandishi wa habari kwamba mwanamke huyo alieleza kuwa alifika hotelini hapo Januari 16, 2021 kama walivyokubaliana na alimkuta marehemu ameshachukua chumba namba 22 akiwa na maji na juisi baada ya kufika aliagiza chipsi na mishikaki mitatu na mzee huyo ambaye baadaye hali yake ilibadilika na kufariki.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments