Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Nandy amkaribisha Koffi, ataja jina la ngoma yao

 


Nguli wa muziki Afrika Koffi Olomide maarufu Mopao, ametua Bongo usiku wa kuamkia leo Januari 26, 2021, kwaajili ya kukamilisha collabo yake na African Princess Nandy.

 


Baada ya kumpokea mgeni wake, Nandy amedokeza jina la ngoma hiyo kuwa ni 'Leo leo' na ameweka wazi kuwa yeye na timu yake wamefanya uwekezaji mkubwa sana kwenye project hiyo, hivyo mashabiki watarajie kitu kikubwa.


''Unajua ili kazi kubwa kama hii ni lazima ufanye vizuri kwahiyo mimi na timu yangu pamoja na timu ya Mopa tumefanya uwekezaji mkubwa sana na naamini tutafanya kitu kikubwa sana na cha tofauti'', amesema Nandy.


Kwa upande wake Koffi ambaye pia amemletea zawadi Nandy ambayo hajaiweka wazi ni nini, amesema ana furaha kufanya kazi na Nandy ambaye ana sauti nzuri sana hivyo mashabiki wa muziki Afrika na Duniani kote wajiandae kwa kazi nzuri.


Nandy na Koffi wanatarajia kuandaa video ya ngoma yao hiyo ambayo taarifa za mwanzo ni kwamba audio yake ilirekodiwa tangu mwaka 2020.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments