Ndugu wa mwanafunzi aliyefariki akijifungua waiomba Serikali iharakishe uchunguzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Serengeti. Ndugu wa Mwanafunzi aliyekufa muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya wilaya ya Serengeti wameiomba Serikali kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo ili ikamilishe mapema.  


Sarah Marwa (13) alifariki Desemba 28, 2020 muda mfupi baada ya kujifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji na ndugu wakagoma kuzika wakishinikiza aliyempa mimba abebeshwe majukumu. 


Marwa Ntatu baba mzazi wa Sarah leo jumamosi Januari 2, 2021 katika eneo la hospitali ya Nyerere wakati wa kufanyia uchunguzi mwili ameiomba serikali isimamie vema kesi licha ya kuwa shahidi namba moja ndiye amekufa ili haki iweze kutendeka.


Amesema walikataa kuzika kutokana na mazingira ya utata wa kifo cha mtoto wake lakini baada ya mjadala mrefu ikiwemo na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo wameridhia kumzika. 


John Magesa kaka wa marehemu amesema kinachowasumbua kwa sasa ni namna ya kumhudumia mtoto mchanga mpaka kukua kwake kwa kuwa anahitaji ulinzi na uangalizi wa hali ya juu. 


"Mimi naomba sana kesi ya mdogo wangu iharakishwe sambamba na matokeo ya uchunguzinwa kujua sababu za kifo chake," amesema.


Dk Damas Ngwegwe mmoja wa waliohusika kufanya uchunguzi wa mwili amesema vipimo vitapelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi. 


Sarah alikatishwa masomo darasa la saba shule ya msingi Kambarage B wakati wa likizo ya Corona 2020 na aliyetajwa kumpa mimba alikamatwa na kesi inaendelea katika mahakama ya wilaya ya Serengeti.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad